Mamia ya wapiganaji wa Urusi na Ukraine wauawa Bakhmut
12 Machi 2023![ARCHIV | Ukraine - Zerstörung in Bachmut nach russischem Luftangriff](https://static.dw.com/image/64119870_800.webp)
Msemaji wa jeshi la Ukraine, Serhiy Cherevatyi, amedai kuwa wapiganaji 221 wanaoiunga mkono Moscow wameuawa na zaidi ya 300 wamejeruhiwa mjini Bakhmut, wakati wizara ya ulinzi ya Urusi ikieleza kuwa wanajeshi 210 wa Ukraine wameuawa katika uwanja wa mapambano mjini Donetsk.
Rais Volodmyr Zelenskiy amesema raia watatu wameuawa katika shambulio la makombora lililofanywa na Urusi mjini Kherson, kusini mwa Ukraine jana Jumamosi.
Rais huyo ameshtumu kile alichokita "mashambulizi ya kikatili" yanayofanywa na wapiganaji wanaiunga mkono Moscow.
Mkuu wa kundi la mamluki wa Urusi, Wagner, Yengeny Prigozhin, alieleza mnamo siku ya Ijumaa kwamba, kundi hili limefungua vituo 42 vya kusajili wapiganaji wapya ili kukiimarisha kikosi chake kufuatia hasara kubwa waliyoipata katika mapambano mjini Bakhmut.