JamiiChina
Mamilioni wajifungia majumbani Shanghai kufuatia kimbunga
16 Septemba 2024Matangazo
Mamilioni ya watu mjini Shanghai na katika maeneo mengine ya China yanayokaliwa na watu wengi ya pwani ya mashariki mwa nchi hiyo wamelazimika kujifungia majumbani mwao Jumatatu, kufuatia kimbunga kikali zaidi kuwahi kulikumba eneo hilo tangu mwaka 1949.
Kimbunga hicho kimesababisha miti kuanguka pamoja na kutatiza usafiri katika eneo zima.
Kimbunga Bebinca kilipiga asubuhi ya Jumatatu katika eneo la pwani ya mashariki ya Shanghai kikiandamana na upepo mkali uliovuma kwa kasi ya zaidi ya kilomita 151 kwa saa,kwa mujibu wa kituo cha serikali cha televisheni cha CCTV.
Wakaazi milioni 25 wa mji wa Shanghai walishauriwa wabakie majumbani mwao.Mvua kubwa imenyesha kufuatia kimbunga hicho huku shughuli za kibiashara zikiwa zimefungwa.