Mamilioni ya dola kutolewa ili kukabiliana na hewa ukaa
4 Septemba 2023Matangazo
Ahadi hizo zimetolewa katika mkutano wa kihistoria wa kilele kuhusu mazingira wa viongozi wa Kiafrika,uliofunguliwa leo na rais wa Kenya William Ruto.
Umoja wa Falme za Kiarabu umeahidi kutowa dola milioni 450 kwaajili ya kusaidia miradi ya masoko ya Kiafrika ya upunguzaji viwango vya uzalishaji hewa ukaa,(ACMI).
Soma pia:Viongozi wa Afrika wakutana kujadili masuala ya mazingira
Mradi wa Masoko hayo ulianzishwa nchini Misri kufuatia mkutano wa kilele wa COP 27 mwaka jana.
Mkuatano wa kilele wa siku tatu wa Nairobi,kwa mujibu wa waandalizi,unalenga kulitangaza bara la Afrika kama kituo cha uwekezaji wa miradi ya kimazingira badala ya kutazamwa kama muhanga wa mafuriko na njaa.