Chad yakabiliwa na kitisho cha ukosefu wa chakula
11 Aprili 2024Masaada huo unahitajika kufuatia kufuatia wimbi kubwa la wakimbizi wanaowasili kutokea Sudan wanakokimbia vita.i
Taarifa ya asasi hiyo imeeleza kwamba majimbo ya mashariki mwa Chad ni miongoni mwa maeneo yaliyo hatarini zaidi nchini humo na upatikanaji duni wa huduma za msingi na kuwasili kwa wakimbizi kumezidisha hali kuwa mbaya.
WFP yafikisha msaada wa chakula Darfur
Mnamo mwezi Machi, Umoja wa Mataifa ulionya kuwa msaada wa chakula kwa maelfu ya watu wanaokimbia mapigano Sudan, utakosekana kufikia Aprili ikiwa hakuna ufadhili wa kimataifa.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani - WFP, limetoa wito wa kukusanywa kwa Dola milioni 242 ili kuepusha janga la kibinadamu na kuendelea kuwahudumia wakimbizi wa Sudan wapatao milioni 1.2.