1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mamlaka Gaza yaonya kuhusu mzozo mkubwa wa kibinadamu

13 Desemba 2025

Mamlaka katika Ukanda wa Gaza imetoa tahadhari leo kuhusu mzozo mkubwa wa kibinadamu katika eneo hilo baada ya dhoruba na mvua kubwa kusababisha mafuriko. Takriban watu 11 wamekufa kufikia sasa.

Gaza-City 2025 | Mafuriko
Mafuriko katika Ukanda wa GazaPicha: Mahmoud Issa/REUTERS

Ofisi ya habari inayoshirikiana na kundi la wanamgambo la Hamas pia imeripoti kuwa nyumba 13 ziliporomoka kutokana na mvua hiyo.

Ofisi hiyo pia imeripoti kuwa zaidi ya mahema 53,000 yaliharibiwa, au kusombwa na maji.

Takriban watu 250,000 kati ya milioni 1.5 wanaoishi katika mahema au makazi ya muda kutokana na vita katika eneo hilo wameathrika .

Hata hivyo ripoti hiyo haikuweza kuthibitishwa kwa njia huru.

Wakati huo huo, Shirika la Umoja wa Mataifa kwa ajili wa kuwasaidia Wapalestina UNRWA limesema kuwa vifaa kwa ajili ya makazi ya dharura kwa hadi watu milioni 1.3 viko tayari nje ya Ukanda huo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW