1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Mamlaka Sudan yawalenga viongozi wa chama cha Kiislamu

1 Agosti 2023

Mamlaka nchini Sudan zinataka kuwakamata tena viongozi wakuu wa chama cha Kiislamu waliotoroka jela katika siku za mwanzo za mapigano, wakati ambapo wapinzani wanaonya kuhusiana na njama zao za kutaka kuchukua madaraka.

Muammar al-Gaddafi - Rais wa zamani wa Libya
Muammar al-Gaddafi - Rais wa zamani wa LibyaPicha: Thomas Imo/photothek/IMAGO

Haya ni kwa mujibu wa nyaraka zilizoonekana na shirika la habari la Reuters. Nyaraka hizo zilizotolewa na mkoa wa Kassala zinataka maafisa wawakamata  Ahmed Haroun, Ali Osman Mohamed Taha na watu wengine watatu ambao walikuwa maafisa waandamizi katika utawala wa miongo mitatu wa Omar al-Bashir.

Vita nchini Sudan vyaonekana kama jaribio la kuibuka kwa udikteta

Wapiganaji wa RSF, wanasiasa na baadhi ya wachambuzi wanasema kwamba vita vya Sudan vilivyodumu kwa zaidi ya miezi mitatu sasa ni jaribio la kuibuka tena kwa utawala wa kidikteta wa al-Bashir. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW