SiasaUrusi
Urusi yaishtumu Ukraine kwa shambulizi
1 Agosti 2023Matangazo
Urusi inasema mojawapo ya droni hizo zimelenga jengo katika mji mkuu ambalo lilikuwa limeharibiwa na droni nyengine siku chache tu zilizopita katika shambulizi sawa na hilo. Wizara ya mambo ya nje ya Urusi imesema mapema leo kwamba imezidungua ndege mbili zisizo na rubani nje ya Moscow.
Urusi yasema Ukraine yaonesha kushindwa kulipiza kisasi
Maafisa wa Urusi wamedai hatua ya Ukraine kuzidisha mashambulizi mjini Moscow inaonesha kushindwa kwake katika kulipiza kisasi. Mwishoni mwa wiki iliyopita, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy alisema kwamba, "vita taratibu vinarudi ndani ya Urusi" ingawa hakukiri kuhusika kwa majeshi yake na shambulizi la droni siku ya Jumapili.