1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAfghanistan

Mamlaka ya Taliban yazima mtandao wa intaneti

30 Septemba 2025

Mamlaka ya Kiislam ya Taliban nchini Afghanistan imeamuru kuzimwa kwa mkongo wa taifa wa intaneti "hadi kutakapotangazwa vinginevyo."

Naibu Waziri Mkuu wa Taliban Abdul Salam Hanafi (katikati) alipozuru karibu na mpaka wa Afghanistan na Pakistan Torkham katika mkoa wa Nangarhar mnamo Aprili 10, 2025.
Naibu Waziri Mkuu wa Taliban Abdul Salam Hanafi (katikati) alipozuru karibu na mpaka wa Afghanistan na Pakistan Torkham katika mkoa wa Nangarhar mnamo Aprili 10, 2025.Picha: AFP

Mapema chanzo cha serikali kilichozungumza na shirika la habari la Ufaransa AFP kwa sharti la kutotambulishwa kilisema hakuna njia au mfumo mwingine wowote wa kuwasiliana na kila sekta itaathirika.

Hii ni mara ya kwanza kuchukuliwa hatua kama hii nchini Afghanistan ambayo itapelekea "kuzimwa kabisa kwa mtandao," hii ikiwa ni kulingana na shirika la NetBlocks la mtandao na usalama wa mtandao lenye makao yake mjini London.

Kundi la Taliban limeanzisha msururu wa vizuizi vya kupambana na "uvinjifu wa maadili" kama unavyofafanuliwa chini ya sheria kali za Kiislamu tangu liliporejea madarakani mwaka 2021.