1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
AfyaUganda

Mamlaka za afya Uganda zatahadharisha juu ya homa ya nyani

2 Julai 2024

Mamlaka za afya nchini Uganda zimetangaza hali ya tahadhari kufuatia mlipuko wa homa ya nyani katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Dalili za maambukizi ya homa ya nyani
Dalili moja wapo za homa ya nyani ni vipele kama hivi, lakini pia homa na maumivu ya misuli. Uganda inaanzisha hatua za tahadhari za kusambaa kwa ugonjwa huo kutoka nchi jirani, Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoPicha: CDC/Getty Images

Kulingana na taarifa za Shirika la Afya Duniani WHO, hadi Mei 26, idadi ya waathirika wa ugonjwa huo ilikuwa imefikia watu 7,851 na 384m wakiwa wamekufa.

Kwa kuwa watu wengi huvuka mipaka kati ya nchi hizo mbili, kuna wasiwasi kwamba huenda mlipuko huo unaweza kufika Uganda na hasa kutokana na wakimbizi wanaokimbilia Uganda kwa ajili ya usalama.

Afisa anayesimamia masuala ya milipuko katika wizara ya afya ya Uganda, Luteni kanali Henry Kyobe amefahamisha kuwa wameanzisha mpango wa kufuatilia watu walioko hatarini kukumbwa na ugonjwa huo, hasa katika wilaya zinazopakana na Kongo, zitakazohusishwa katika mpango wa kufuatilia afya za watu wanaoingia Uganda, ambao hawajafikia hatua ya kuwekwa karantini.

WHO limesema ugonjwa huo huambukizwa kutoka kwa wanyama na dalili zake ni vipele, homa kali, maumivu ya kichwa na misuli.

Maafisa wa Uganda wamesema ugonjwa huo pia una madhara makubwa kwa akina mama wajawazito na unaweza kusababisha mimba kuharibika.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW