1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Mamluki wa Wagner wameanza kujiondoa Bakhmut

2 Juni 2023

Yevgeny Prigozhin amesema wapiganaji wake wameanza kujiondoa katika viunga vya mji wa mashariki wa Ukraine wa Bakhmut.

Russland Jewgeni Prigoschin Bachmut Wagner
Picha: PRESS SERVICE OF "CONCORD"/REUTERS

Kiongozi wa kundi la wapiganaji mamluki la Kirusi-Wagner, Yevgeny Prigozhin amesema wapiganaji wake wameanza kujiondoa katika viunga vya mji wa mashariki wa Ukraine wa Bakhmut.

Akizungumza kupitia mkanda wa video kiongozi huyo amesema mpaka kufikia Juni 5  maeneo yote ya uwanja wa mapigano watakuwa wameyakabidhi kwa jeshi la Urusi.

Hata hivyo Prigozhin amesema watajiondoa katika maeneo hayo ya mstari wa mbele lakini wataendela kuweka kambi katika mji mwingine wa mashariki mwa Ukraine wa Donetsk.

Kwa upande wake kamanda wa vikosi vya ardhini wa Ukraine, Oleksandr Syrskyi jeshi lake limesimamisha mapigano katika maeneo ya Bakhmut na wanajipanga upya ili kushirika mapigano hayo kwa mbinu sahihi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW