Man city sasa kushiriki Champions League msimu ujao
13 Julai 2020Matangazo
Mahakama ya usuluhishi wa mizozo ya michezo imeikubali rufaa ya Manchester City dhidi ya marufuku ya UEFA kwa klabu hiyo kutoshiriki mechi za kombe la mabingwa barani Ulaya Champions League kwa misimu miwili kuanzia msimu ujao. Ila City wametozwa faini ya yuro milioni 10 kwa kutoshirikiana na wachunguzi katika suala hilo.
Uamuzi huo wa majaji watatu unawanadhifisha City iliyo chini ya ukufunzi wa Pep Guardiola kushiriki Champions League msimu ujao. Uamuzi huo hauathiri kivyovyote nafasi ya klabu hiyo kwenye mashindano ya msimu huu.