1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
KandandaUlaya

Carrick kuendelea kuinoa United

9 Novemba 2026

Michael Carrick amesisitiza kuwa hatajiuzulu kama kocha wa Manchester United baada ya sare ya 4-4 dhidi ya Aston Villa.

Uingereza, Manchester 2025 | Manchester United vs. ACF Fiorentina | Bryan Mbeumo
Mshambuliaji wa Manchester United Bryan MbeumoPicha: Matt McNulty/Getty Images

Sare hiyo ya ligi kuu inahakikisha kuwa United watakuwa katika hatari ya kushuka daraja kwenye kipindi chote cha mapumziko ya mechi za kimataifa.

Magoli ya dakika za mwisho kutoka kwa Joshua Zirkzee na Patrick Dorgu yaliwapelekea United kupata pointi moja katika siku ambayo walianza mechi hiyo kwa kukubali magoli mawili ya mapema kabisa katika kila kipindi.

United wako kwenye nafasi ya 18 kwa sasa wakiwa na pointi nane na wamekwenda mechi nane bila kupata ushindi hata katika mechi moja hiyo ikiwa ni rekodi wameiweka katika enzi ya Ligi ya Premier.

Kuachia ngazi hakuko akilini mwangu

Alipoulizwa iwapo ataachia ngazi kama hicho ndicho kitu sahihi cha kufanya, Carrick alijibu, "hicho hakiwezi kufanyika."

Shabiki wa Aston Villa akifuatilia mechiPicha: Mark Enfield/IPS/IMAGO

Kocha wa Villa Unai Emery ambaye amekuwa akidaiwa kuwa ni mmoja wa makocha wanaowindwa ili kuichukua nafasi ya Carrick, alighadhabishwa na timu yake kukubali bao la kusawazisha na kumpelekea kukosa kuvunja rekodi ya kutofiunga Manchester United ugenini katika taaluma yake ya kocha.

"Muamuzi aliongeza dakika sita, nafikiri mechi ilikuwa imekwisha," alisema Emery. "Nimekasirika bila shaka. Kukubali kupoteza katika dakika sita za mwisho za mechi ni jambo gumu mno..."

Dorgu ndiye aliyefunga goli la kusawazisha katika dakika ya mwisho ya mechi na Emery amekiri kwamba mlinda lango wake Zion Suzuki ambaye ameridhisha kimchezo tangu ajiunge na Villa mwanzoni mwa msimu, bado ana mengi ya kujifunza.

Imehaririwa na:Babu Abdalla
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW