1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Man United wawania nafasi ya tatu ligi ya Premier

Sekione Kitojo
24 Julai 2020

Manchester United imehimili kipindi cha matatizo katika msimu wa ligi ya Uingereza Premier League lakini kufika nafasi ya tatu kwa ushindi dhidi ya Leicester City Jumapili itakuwa ushahidi zaidi wa uwezo wa kikosi hicho.

Manchester United-Trainer Ole Gunnar Solskjaer
Picha: Getty Images/C. Ivill

Solskjaer  ameiongoza  timu  hiyo  ya  Old Trafford katika  mwanzo mbovu  kabisa  katika  kampeni  ya  ligi  hiyo katika  muda  wa  miaka 30 na  kukabiliwa  na  maswali  juu  ya  uwezo  wakw  kwa  ajili  ya ujenzi  mpya wa kikosi cha  klabu  hiyo,  lakini  kikosi  cha  vijana  wa United kilibadilisha  mambo  katika  sehemu  ya  pili  ya  msimu.

Baada  ya  kwenda  bila  kufungwa  katika  michezo  13 ya  ligi , United inaweza  kupata nafasi  yao  ya  juu  kabisa  tangu  msimu wa  mwaka  2017-18  wakati  Jose Mourinho alipoiongoza  timu  hiyo na  kufikia  nafasi  ya  makamu  bingwa.

Kikosi cha Manchester UnitedPicha: picture-alliance/dpa/empics/M. Rickett

"Ngoja  tumalize  mchezo huu na  kupata  nafsi  ya  tatu  na kuendeleza  ukuaji wetu na  safari  ambayo  timu  hii  inaelekea. Tumekuwa  na  nyakati  ngumu msimu  huu, baadhi  ya vikwazo, lakini  tumeonesha  kuwa  timu  hii  inakwenda  mbali," Solskjaer aliwaambia  waandishi  habari.

Solskjaer , ambaye  timu  yake  ilionja chungu  ya  kufungwa  katika mashindano  dhidi  ya  Burnley mwezi  Januari, amesema kuongezwa  kwa  mchezaji  wa  kiungo  Bruno Fernandes ni miongoni  mwa  sababu  za  mafaniko  yao.

Marcus Rashford mshambuliaji wa kutumainiwa wa Manchester UnitedPicha: Imago Images/R. Hart

Solskjaer  amesema  kwamba  lengo  lao  kuu ni  kunyakua  pointi tatu  muhimu  katika  mchezo  dhidi  ya  timu  iliyoko  katika  nafasi ya  tano Leicester City.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW