MANAMA: Iran ipo tayari kuisaidia Marekani kuondosha vikosi Irak
9 Desemba 2006Matangazo
Waziri wa mambo ya nje wa Iran Manouchehr Mottaki amesema,Iran ipo tayari kuisaidia Marekani kuhamisha vikosi vyake kutoka Irak,ikiwa Washington itabadilisha msimamo wake kuhusu Iran. Alipozungumza nchini Bahrain,waziri Mottaki alisema,vikosi vya kigeni vilivyoikalia Irak vinabeba lawama ya takriban nusu ya machafuko yanayotokea nchini humo.Kwa maoni ya Mottaki,eneo zima litanufaika kama Marekani itaviondosha vikosi vyake kutoka Irak.