1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mandamano makubwa yafanyika katika mkutano wa COP30, Brazil

15 Novemba 2025

Maandamano makubwa yamefanyika leo katika Mkutano wa UN wa Mazingira (COP30) nchini Brazil. Maelfu ya watu wa jamii za asili na wanaharakati wa kimataifa wa hali ya hewa, waliandamana katikati ya jiji la Belém.

Brazil Belém 2025 | wanaharakati wa mazingira waandamana
Maandamano ya wanaharakati katika mkutano wa COP 30 nchini BrazilPicha: Igor Mota/ZUMA/picture alliance

Katika maandamano hayo yaliyopewa jina'' Maandamano kwa ajili ya Hali ya Hewa," waandamanaji wanadai haki katika suala zima la hali ya hewa na ulinzi wa ardhi ya jamii za asili ambazo ziko hatarini kutokana na ukataji miti na uchimbaji haramu wa dhahabu.

Tofauti na wakati wa mikutano ya hali ya hewa iliyopita katika mataifa kama vile Azerbaijan, maandamano yameruhusiwa kufanyika nchini Brazil wakati mazungumzo yakiendelea.

Hapo jana, watu kadhaa wa jamii za asili na wanaharakati wengine wa hali ya hewa walifunga lango kuu la kuingilia mkutano huo kwa saa kadhaa.

Katika mkutano huo wa COP30, takriban nchi 200 bado zinajadili hadi mwisho wa wiki hii namna ya punguza ongezeko la joto duniani kwa haraka zaidi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW