1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mane awasili Munich kukamilisha uhamisho kutoka Liverpool

21 Juni 2022

Mshambulizi wa pembeni wa timu ya taifa ya Senegal Sadio Mane amewasili mjini Munich leo Jumanne kukamilisha uhamisho kutoka Liverpool na kujiunga na mabingwa wa ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga, Bayern Munich.

Champions League I Villareal CF v Liverpool
Picha: Alberto Saiz/AP/picture alliance

Shirika la Habari la Sky TV limemuonyesha Mane akiwasili kwa ndege binafsi kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya kusaini kandarasi ya miaka mitatu ya kuichezea Bayern.

Gazeti la michezo la Kicker limesema mchezaji huyo atatambulishwa rasi kesho Jumatano.

Hata hivyo, Liverpool na Bayern Munich bado hazijathibitisha uhamisho huo japo klabu hizo zinaripotiwa kukubaliana dau la uhamisho la pauni milioni 33.7, ambalo linaweza kupanda hadi pauni milioni 41 ukijumuisha na marupurupu.

Mane mwenye umri wa miaka 30 anatarajiwa kuimarisha safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo yenye makao yake Allianz Arena hasa baada ya kuibuka fununu kwamba Serge Gnabry na Robert Lewandowski huenda wakaondoka klabuni humo katika dirisha la uhamisho la majira ya joto.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW