1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MANILA : Arroyo aendelea kukaata wito wa kujiuzulu

9 Julai 2005

Rais Gloria Arroyo wa Ufilipino amewatangaza mawaziri sita wapya wakati mgogoro wa kisiasa nchini humo ukizidi kupamba moto.

Hatua yake hiyo inakuja baada wajumbe wanane wa timu yake ya uchumi kujiuzulu na kumtaka naye pia ajiuzulu. Rais Arroyo amekuwa akikabiliwa na madai ya kujaribu kushawishi matokeo ya uchaguzi wa rais mwaka jana.Alikiri kuzungumza na afisa wa uchaguzi kufuatia uchaguzi huo wa mwaka jana lakini amekanusha kujaribu kushawishi kinyume na sheria matokeo ya uchaguzi huo.

Hadi sasa kiongozi huyo amekuwa akigomea wito unaomtaka ajiuzulu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW