1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MANILA: Kimbunga Durian kimeua mamia nchini Ufilipino

2 Desemba 2006

Chama kinachotoa msaada cha Msalaba Mwekundu nchini Ufilipino kinasema,takriban watu 400 wameuawa katika mporomoko wa matope uliosababishwa na kimbunga cha Durian.Wengine 96 hawajulikani walipo na vijiji vingi karibu na mlima Mayon kama kilomita 320 kusini-mashariki ya mji mkuu Manila,vimegubikwa na matope na mawe yalioporomoka kufuatia mvua kali zilizosababishwa na kimbunga Durian.Idadi ya vifo inatazamiwa kuongezeka huku ripoti zikipatikana kutoka maeneo yasio na mawasiliano.Durian ni kimbunga cha nne kuikumba Phillipines katika kipindi cha miezi mitatu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW