1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MANILA. Mungu amuweke pema kadinali Sin

21 Juni 2005

Kadinali Jaime Sin wa kanisa katoliki mjini Manila Ufilipino ameaga dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Habari za kifo chake zimetangazwa na maafisa wa kanisa katoliki na wakasema kuwa kadinali Jaime Sin mwenye umri wa miaka 76 alifariki kutokana na maradhi ya figo.

Kadinali Sin alipaaza kwenye vyombo vya habari vya kimataifa mwaka 1986 alipo waongoza watu milioni moja mjini Manila kujenga ukuta wa kibinadamu ili kuwalinda wanajeshi waasi ambao hatimae walifaulu kumpindua dikteta Ferdinand Marcos aliyelaumiwa kwa kuthiri vitendo vya rushwa na uvunjaji wa haki za kibinadamu wakati wa utawala wake nchini Ufilipino.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW