Manila. Uchaguzi wa bunge wamalizika.
14 Mei 2007Nchini Philippines , vituo vya kupigia kura vimefungwa baada ya uchaguzi mdogo , ambao ulikuwa na madhumuni ya kuwachagua wabunge wapya 275 wa baraza la wawakilishi , magavana wa majimbo na meya wa miji mbali mbali.
Ghasia zimetia doa katika kampeni, na kusababisha watu sita kuuwawa leo Jumatatu, pamoja na watu 116 ambao wameuwawa tangu Januari mwaka huu.
Waandishi wa habari wanasema kuwa baraza la wawakilishi linaweza kubaki katika udhibiti wa wale wanaomuunga mkono rais Gloria Macapagal Arroyo.
Baadhi ya waandishi wanasema kuwa vyama vya upinzani vinataka kujiweka tayari kwa uchaguzi mkuu wa rais.
Amekabiliana na juhudi za kumshitaki kuhusiana na madai kuwa alipanga wizi wa kura katika uchaguzi wa mwaka 2004.
Wafilipino pia wanachagua wabunge 12 kati ya 24 wa baraza la Seneti, ambapo wapinzani wamekuwa wengi.