Manila. Viongozi wakubaliana mkataba wa kupambana na ugaidi.
14 Januari 2007Matangazo
Viongozi wa mataifa ya kusini mashariki ya Asia, wametia saini makubaliano muhimu ya kupambana na ugaidi.
Katika mkutano wao wa kila mwaka katika kisiwa cha Philippines cha Cebu, viongozi hao wa chama cha mataifa ya kusini mashariki ya Asia wamekubaliana na mkataba huo unaowalazimisha kisheria na kufanya kuwa mkataba wa kwanza wa eneo hilo.
Mkataba huo unayataka mataifa hayo ya Asia kuimarisha uhusiano wao wa kuzuwia na kuchunguza mashambulizi ya kigaidi. Mataifa hayo 10 pia yamekubaliana kupeleka mbele muda wa lengo la kufikiwa eneo hilo kuwa la biashara huru hadi mwaka 2015.