1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MANILA Wafuasi wa rais Arroyo wafanya maombi mjini Manila

16 Julai 2005

Maelfu ya wafuasi wa rais Gloria Arroyo nchini Ufilipino wamehudhuria mkutano wa maombi mjini Manila, wakitaka aendelee kubakia madarakani.

Rais Arroyo anashinikizwa ajiuzulu kutoka kwa wadhfa wake, tangu upinzani ulipotoa ukanda wa sauti, ambamo mwanamke mwenye sauti inayofanana na yake, anasikika akijaribu kuomba apendelewe wakati kura zilipokuwa zikihesabiwa, kufuatia uchaguzi wa urais mwaka jana.

Arroyo amepinga kufanya kitendo hicho na msemaji wake Ignacio Bunye amesema hatakubali kuteswa na upinzani. Mawaziri wanane wa baraza lake la mawaziri wamejiuzulu kufutia mzozo huo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW