1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MANILLA Watu wawili wakamatwa nchini Ufilipino.

23 Februari 2005

Watu wawili wanaotuhumiwa kuwa magaidi wametiwa mbaroni nchini Ufilipino. Polisi wanadai wanachama hao wa kundi la Abu Sayyaf, lenye uhusiano na kundi la kigaidi la al-Qaeda, walitega bomu ndani ya basi la abiria siku ya sherehe za wapendanao, katika mji mkuu Manilla. Mripuko uliotokea uliwaua watu sita na kuwajeruhi wengine zaidi ya mia moja. Kundi la Abu Sayyaf lilidai lilitekeleza mashambulio mengine mawili ya bomu siku hiyo ya Valentine katika miji ya kusini ya General Santos na Davao, ambayo yalipelekea kuuwawa kwa watu wengine sita na kuwajeruhi wengine wengi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW