1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Manuel Neuer atangaza kustaafu soka la kimataifa

21 Agosti 2024

Na katika michezo, mlinda lango wa timu ya taifa ya Ujerumani Manuel Neuer ametangaza leo kustaafu soka la kimataifa baada ya kuichezea timu hiyo mechi 124 tangu mwaka 2009.

Kipa wa Ujerumani Manuel Neuer katika kombe la dunia lilichezwa Qatar
Kipa wa Ujerumani Manuel Neuer katika kombe la dunia lilichezwa QatarPicha: Frank Hoermann/SVEN SIMON/picture alliance

Neuer, mwenye umri wa miaka 38 ameandika kwenye mtandao wake wa Instagram kwamba leo ndio mwisho wake wa kuichezea timu ya taifa ya Ujerumani. Mchezaji huyo wa Bayern Munich alishinda tuzo ya kipa bora wakati Ujerumani Die Mannschaft iliposhinda Kombe la Dunia mnamo mwaka 2014. Amesema amefikiria kwa muda mrefu kabla ya kuamua kustaafu soka la kimataifa na kwamba huu ndio muda mwafaka wa kufunga kurasa na timu yake ya taifa. Shirikisho la soka la Ujerumani DFB limemueleza Neuer kama moja wa makipa bora duniani.Tangazo la Neuer limetokea siku mbili tu baada ya kiungo na nahodha Ilkay Gundogan pia kuchukua uamuzi kama huo wa kustaafu soka la kimataifa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW