1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Manusura waomba msaada baada ya ajali ya Meli nchini Kongo

Saleh Mwanamilongo
16 Oktoba 2023

Juhudi za kutafuta manusura zinaendelea jimboni Equateur Kaskazini magharibi mwa Kongo baada ya ajali ya Meli iliosababisha vifo vya watu wasiopungua 40 na wengine zaidi ya mia moja kutoweka.

Watu wasiopungua 157 wametoweka baada ya ajli ya Meli jimboni Equateur
Watu wasiopungua 157 wametoweka baada ya ajli ya Meli jimboni EquateurPicha: Junior Kannah/AFP/Getty Images

Naibu gavana wa jimbo la Equateur, Taylor Ng'anzi ameiambia redio ya Umoja wa mataifa nchini Kongo, Radio Okapi, kwamba wanahitaji msaada wa haraka kuwaokoa manusura. Pia amesema msaada huo utawawezesha kusaidia manusura ambao wamepoteza kila kitu na kurahisisha kurejea makwao. Serikali ya mkoa wa Equateur pia inanuia kutoa huduma za kisaikolojia kwa watoto waliojeruhiwa ambao walipoteza wazazi wao wakati wa ajali hiyo ya meli.

Siku tatu bada ya tukio, juhudi za kuwatafuta manusura zinaendelea. Naibu gavana wa Jimbo la Equateur, Taylor Ng'anzi amesema maiti iliopatakana hadi jumapili jioni kwenyer mto Kongo imezikwa mjini Mbandaka, mji mkuu wa jimbo hilo la Equateur.

Ngazi alisema hivi sasa wanaendelea na kutafuta pia familia za watu waliofariki pamoja na za manusura ili kurejesha baadhi ya bidhaa zilizookolewa kwenye meli hiyo.

Kuanzishwa kwa uchunguzi

Safari hatarishi za majini nchini KongoPicha: picture alliance / dpa

Mashuhuda wamesema mashua hiyo ya HB Mapamboli iliosafiri kutoka Mbandaka kwenda Bolomba umbali wa kilomita mia moja hakiufanikiwa kusonga mbele kutokana na uzito wa kupita kiasi. Mashua ilizama dadika chache chuu baada ya kuanza safari yake.

Viongozi wa jimbo la Equateur wametangaza kuanzishwa kwa uchunguzi wa ajali hiyo.

Asasi moja ya kiraia imesema idadi ya vifo huenda ikaongezeka. Joseph Boyoko Lokondo, kiongozi wa shirika la kiraia la "Generation consiente" amesema wameorodhesha vifo 50.

Ajali za meli za mara kwa mara nchini Kongo zliibua mjadala kwenye kikao cha bara la mawaziri Ijumaa jioni. Rais Felix Tshisekedi aliiomba serikali yake kuhakikisha kwamba ajali za aina hiyo hazitokee tena. Huku akihimiza kuweko na vifaa vya kisasa vya usafariki mwa majini kote nchini.

Kauli ya upinzani

Huku Kongo ilielekea kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu wa hapo Desemba, ajali hiyo ya meli imemulikwa pia kisiasa. Upinzani haukusita kuilaamu serikali kwa kushindwa kuwakinga raia wake. Kwenye mtandao wake wa X, moja ya wagombea wa urais kutoka Upinzani, Moise Katumbi amesema serikali ndio ya kulaumiwa kwa kuruhusu meli zilizochakaa kuwabeba wananchi na kuhatarisha maisha yao.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW