1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maombolezi ya wahanga wa ADF Kongo Mashariki

Admin.WagnerD18 Mei 2016

Katika kuwakumbuka maelfu ya raia waliouawa na waasi wa Uganda ADF kwa kukatwa mapanga wilayani Beni, katika kipindi cha miaka karibu miwili, mashirika ya kiraia mashariki mwa DRC yameitisha siku tatu za maombolezi.

Martin Kobler
Picha: John Kanyunyu

Kwa kipindi cha siku tatu hizo, raia wa mji na wilaya ya Beni, wilaya ya Lubero na mji wa Butembo wanabaki majumbani, na magari pamoja na helikopta za tume ya Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo pamoja na magari ya mashirika ya kiutu ya kimataifa, hayaruhusiwi kuzunguka katika eneo hilo. Sikiliza ripoti ya John Kanyunyu kutoka Beni hapo chini.

Mhariri: Mohammed Abdul-Rhman

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi

Gundua zaidi

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW