1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maonesho ya ajira kati ya Ujerumani na Kenya yafunguliwa

Shisia Wasilwa
27 Septemba 2024

Akizungumza wakati wa Kongamano la Uhamiaji na Maonesho kati ya Kenya na Ujerumani jijini Nairobi, Waziri wa Ajira nchini Kenya Alfred Mutua alisema kuwa mashirika ya mawakala yatakaokiuka sheria yatafutiliwa mbali.

Balozi wa Ujerumani nchini Kenya Sebastian Groth na waziri wa Kazi wa Kenya Alfred Mutua (wa tatu-kushoto) wakati wa mkutano uliofanyika Nairobi.
Balozi wa Ujerumani nchini Kenya Sebastian Groth na waziri wa Kazi wa Kenya Alfred Mutua (wa tatu-kushoto) wakati wa mkutano uliofanyika Nairobi.Picha: Shisia Wasilwa/DW

Kwenye kongamano la Uhamiaji na maonesho lililoandaliwaa jijini Nairobi, ilibainika kuwa katika kipindi cha miezi mitatu ijayo serikali inatarajiwa kupokea maombi 500 ya Wakenya wanaopanga kuajiriwa Ujerumani.

Waziri wa Ajira nchini Kenya Alfred Mutua amesema kuwa serikali itaweka mikakati ya kufidia mawakala ambao watawasaidia wakenya kupata ajira Ujerumani. Mutua amesema, "Tutafutilia mbali mawakala walaghai. Wazazi wanauza mali kuwasaidia watoto kupata ajira kisha wanaachwa wakitaabika baada ya kudanganywa na mawakala wakora. Muanze kujiandaa kwa sera mpya ambapo  mawakala hawatawatoza ada zozote.”

Soma: Ujerumani na Kenya zasaini mkataba wa uhamiaji na ajira

Mutua aliongeza kusema kuwa, serikali itayafutilia mbali mashirika ya mawakala yatakayokiuka kanuni na sheria za nchini. Kwenye kongamano hilo ilibainika pia, serikali itaanza kuwahamasisha Wakenya kote nchini ili wafahamu masharti ya kuhudumu katika taifa la Ujerumani.

Viongozi wa Kenya na Ujerumani wakishuhudia utiaji saini wa makubalianoPicha: Maja Hitij/Getty Images

Mashirika kadhaa ya mawakala yameripotiwa kuwalaghai Wakenya wanaotaka kusafiri nje ya Kenya kwa ajira. Mutua alisema kuwa serikali itazikagua upya leseni za mashirika yatakayohusika kwenye mchakato wa maombi ya kazi nchini Ujermani. 

Kwa upande wake Balozi wa Ujerumani nchini Kenya Sebastian Groth, alipuuzilia mbali suala la Maarifa ya Wakenya kupotelea ughaibuni. Sebasitain amesema, "Sehemu moja ya sarafu ni kuchocheampango wa kuhamisha wafanyikazi wenye ujuzi na sehemu nyingine ni kuhamisha watu ambao hawana uraia kwenye taifa.”

Soma: Ruto atetea rikodi ya uongozi wake wa miaka miwili

Kenya inakabiliwa na matatizo yanayoongezeka katika kutoa ajira na mapato ya kutosha kwa wataalamu wake wachanga, huku Ujerumani ikikabiliwa na uhaba wa wafanyakazi wenye ujuzi.

Mahojiano maalumu na Rais William Ruto wa Kenya

12:24

This browser does not support the video element.

Asma Rashid ni mmoja wa baadhi ya vijana walio na ndoto za kuelekea Ujerumani kufanya kazi. Anasema, "Changamoto ninayopitia kama kijana ni kuwa ninapotafuta kazi nje ya nchi nakutakana na walaghai ambao wanataka kunipunja hela.”

Mikataba ya uhamiaji ni nguzo kuu katika juhudi za serikali ya Ujerumani kuzuia uhamiaji. Mkataba huo pia utarahisisha urejeshwaji wa Wakenya walioko Ujerumani bila kibali cha kisheria.

Shirika la Kazi Duniani (ILO) lilisema mpango huo unatarajiwa kuongeza kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa kazi za heshima za kigeni kwa wafanyikazi wa Kenya nchini Ujerumani na kushughulikia uhaba wa wafanyikazi nchini Ujerumani.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW