1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wachochezi hawajali

3 Novemba 2015

Makundi ya siasa kali za mrengo wa kulia yanadhihirika kupata nguvu kutokana na mikururo ya wakimbizi wanaozidi kuingia humu nchini na mivutano miongoni mwa vyama vikuu, juu ya namna ya kulipatia ufumbuzi tatizo hilo.

Wagener,Volker

Hata si muda mrefu hivyo,hivi karibuni tu,tulipofifiisha vitisho vyote dhidi ya mfumo wetu wa demokrasia na kuvitajakuwa ni mizingo ya kisiasa.Sisi wenyewe tunaojiita wanademokrasia mahiri-wapiga kura tuliobobea na wenye kuheshimu sheria msingi-tulikuwa hatujui nini cha kufanya kutokana na kuzidi ushupavu miongoni mwa jamaa,marafiki na majirani na kutozingatia chochote kinachosemwa na serikali au na jamii .

Hii leo,mbele ya wakimbizi wanaotarajiwa kufikia milioni moja,jamhuri inaonyesha kupoteza hali ya kujiamini.Tunajikuta ukingoni mwa hali ya hatari na makundi ya watu wanaitumia hali hiyo.Makundi ya siasa kali za mrengo wa kulia wanapalilia,wakifuatwa na wale waliokuwa wakifanya vituko vya kichini chini na ambao hivi sasa wameamua kufunua sura zao.

Wiki chache tu zilizopita sisi ndio tuliokuwa watu wazuri.Tukipenda utamaduni na kuwa wakarim.Hivi sasa sisi ndio tunaoongoza madaftari kuhusu mashambulio na hujuma dhidi ya wasiojiweza.Mjini Cologne mgombea waadhifa wa meya akachomwa kisu,vituo vya kuwapokea wakimbizi vikatiwa moto-wanazi mambo leo wawili wakawakojolea watoto wenye asili ya kigeni.Uchunguzi umeonyesha kua asili mia 70 ya visa vya uhalifu mpaka sasa bado polisi hawajui vimefanywa na nani.Kwanini?

Hata wahalifu wa muda mrefu hawana hofu

Lakini hata wahalifu wa muda mrefu wanaonyesha hawauogopi mkono mkali wa serikali.Kwasababu mkono kama huo haupo.Ikilinganishwa na nchi nyengine za Umoja wa ulaya Ujerumani inaangaliwa kuwa mpole katika kukabiliana na visa vya "uhalifu unaosababishwa na chuki ."Hatua zinazofuatwa tangu miongo kadhaa nchini Marekani na Uengereza upande huo,hazifuatwi hivyo humu nchini.Ingawa hata humu nchini waendesha mashtaka na mahakimu wangeweza mara nyingi kuingilia kati,lakini hawafanyi hivyo-wamefafanua waasisi wa uchunguzi wa taasisi moja ya serikali kuu inayopambana na visa vya uhalifu.Na kwanini?Hii hali ya upole ya taifa linaloheshimu sheria mbele ya wafanya fujo wanaotoa maneno ya kibaguzi inaonyesha kuwapa kichwa wafuasi wa asiasa kali za mrengo wa kulia na kuwaambukiza pia "wananchi wenye hishma zao."

Damkorsaia lazma ijihami

Hata maafisa wa idara za upelelezi wanaonyesha kuwavumilia kidogo wachochezi wa siasa kali za mrengo wa kulia.Pegida wanajulikana lakini hawachunguzwi.Kana kwamba maandamano ya kila jumatatu ya mjini Dresden ni zoezi la kidemokrasi la raia wanaolalamika hadharani.Wanajikuta majiani hawakosi kujiambia:kumbe tuko wengi eh!Hili ni tukio la saikolojia ya jamii.Mmoja akianza choko choko atakuta na wengine hawako mbali na hapo.Wale ambao hadi sasa walikuwa watulivu,wameanza kwa ghafla kusema kile ambacho daima walikuwa wakikifikiria.Wanaidharau serikali na mfumo wa demokrasia na wanasubutu kujiita eti "wajerumani wanaoyasema mambo namna yalivyo."

Ndio maana lilikuwa kosa pale waziri wa sheria Heiko Maas alipokataa kuwaandama kisheria wale waliomlinganisha na mweneza propaganda wa Hitler Goebbels.Bila ya shaka katika wakati kama huu kutolewa maelezo ni jambo la maana kuweza kuzuwia balaa lisipate nguvu.Lakini kama nyumba imeshaanza kuungua,hatuwezi tena kutafuta bima ya vilivyomo ndani ya nyyumba.Kilichobakia hivi sasa ni kupiga vita hisia za chuki na matumizi ya nguvu.Demokrasia lazma ijihami tena kwa nguvu zote zilizoko.Kwasababu kimoja ni dhahir,demokrasia ya Ujerumani inaweza kumudu vyema zaidi kishindo cha wakimbizi-kimakaazi na kifedha kuliko hatari inaoweza kutokana na makundi ya wanaoneza chuki katika jamii.

Mwandishi:Wagener,Volker/Hamidou Oummilkheir

Mhariri : Mohammed Abdul-Rahman