1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni: EU yajaribu kuweka hai mkabata wa kinyuklia na Iran

Sekione Kitojo
18 Mei 2018

Bila shaka Umoja wa Ulaya una uwezo wa kupambana  na Marekani. Kwa mfano: Miaka 22 iliyopita Marekani ilitaka kulilazimisha taifa  la  Cuba kuipigia magoti, lakini mataifa ya Ulaya yaligoma kuifuata Marekani.

Bulgarien EU-Balkan-Gipfel in Sofia | Jean-Claude Juncker
Picha: Reuters/S. Nenov

Mataifa  ya  Umoja  wa  Ulaya yamechukua  hatua  kuyaruhusu  makampuni  ya  Ulaya kukwepa  vikwazo  vya  Marekani  dhidi  ya Iran katika  kile kinachojulikana  kama "sheria  inayozuwia".

Tofauti  na  wakati  huu, wakati  ule rais  wa  Marekani alikuwa  Bill Clinton, lakini  leo  inajulikana. Pamoja  na hayo  Umoja  wa  Ulaya  unaweza  kuyalinda  makampuni yake  dhidi  ya  kitisho  cha  vikwazo  vya  Marekani  na kuzuwia  athari zake.

Pia uwekezaji  rasmi  ama misaada  rasmi  kupitia uwekezaji  wa  makampuni  ya  binafsi  unawezekana. Umoja  wa  Ulaya pia  kupitia vyombo  hivyo unaweza kuingia  katika  mapambano  na  Trump.

Ni  kwa  njia  hiyo  tu  makampuni  ya  Ulaya  yanaweza kufanyakazi,  katika  nchi  ambayo  inalengwa  na Marekani  katika  mtazamo wake  kama  inavyoonekana kwa  Iran.  Sasa  linabakia  swali  tu  iwapo  mataifa  ya Ulaya  na  viongozi  wao  wako tayari  kuingia  ulingoni kuitetea  Iran. 

Kila  konde la  nguvu  litakalotoka  upande  wa  Umoja  wa Ulaya  kuelekea  Marekani  linaweza  kuzidisha mapambano  zaidi, na  kuelekeza katika uharibifu  mkubwa zaidi  wa  kiuchumi. Hata  ilipofika Jumanne  jioni hakukuwa  na  ishara  ya  matumaini  makubwa, kwamba viongozi  wa  Ulaya  wako  tayari, kuelekea  katika  njia  hii.

Muandishi wa maoni haya Max HofmannPicha: DW

Makampuni yanauchaguzi

Kwa  hali  hiyo  makampuni  makubwa  ya  kibiashara kama  Siemens  yanatarajia  kuchukua  uamuzi, kama kufanyakazi  na  Iran  ama  kuwekeza  zaidi na   kujiingiza katika mgogoro na   Marekani.  Huenda pengine  ikawa fursa  sahihi  kwa  ajili  ya  mwelekeo  wa  makampuni hayo, kwamba  biashara  na  Marekani  kwa  wengi ni muhimu  sana.

Kwa  upande wa  kampuni  la  Siemens  kwa  mfano Marekani  ndio soko  lake  kuu.  Kwa  Umoja  wa  Ulaya huu  ni  utata  mkubwa, kwani wanahitaji  makampuni  ya watu  binafsi, kuweza  kufanikisha  uwekezaji  nchini  Iran, uwekezaji  ambao  unahitajika  mno. Lakini  Umoja  wa ulaya hauwezi  kuyalazimisha  makampuni, kufanyakazi nchini  Iran. Mataifa  yaliyobaki  ambayo  yalitia  saini makubaliano  ya  kinyuklia  na  Iran, bado yanajaribu kutafuta  njia.

Lakini  hata  hivyo  kuna  matatizo.  Urusi  kwa  mfano inataka  kutekelezwa  kwa  kina  makubaliano  hayo,  wakati kiuchumi  ni  mshindani  mkubwa  wa  Iran. Mataifa  hayo yote yanategemea  sana biashara  ya nje ya mafuta. Na kwa upande wa China kwa  kweli  ina  mambo  yake  ya kufanya  badala  ya  kujiingiza  katika  mapambano  katika jambo  hili na  Marekani.

Kwa  hivi  sasa  China  inajaribu  kuzuwia  vita  vya kibiashara  na   utawala  wa Trump. Katika  suala  hili  la mkataba  na  Iran  kwao  lina  umuhimu  mdogo.

Mwandishi: Max Hofmann / ZR / Sekione Kitojo

Mhariri: Josephat Charo

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW