1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni: Hutatembea peke yako - mkutano wa waandishi na Scholz

12 Agosti 2022

Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani amefanya mkutano wake wa kwanza wa majira ya kiangazi na waandishi wa habari katika dakika 100 ambazo Christoph Strack anasema zilionesha jinsi kiongozi huyo anavyojiamini.

Sommer-Pressekonferenz Bundeskanzler Olaf Scholz
Picha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Suala hili kwa hakika lilikuwa ndilo jambo muhimu zaidi kwa Kansela Scholz. Alitaka kuwahakikishia raia. Nchi itavuuka kwenye nyakati hizi ngumu, hakuna atakayeachwa apambane na matatizo peke yake, hatazamii kutakuwa na machafuko ya kijamii. Kwa ujumla, ilikuwa kama anasema: Musiogope!

Kwa mara ya kwanza, Scholz amehudhuria mkutano huu akiwa mkuu wa serikali katika ukumbi wa mikutano mjini Berlin, eneo linalotegemewa kuwa la masuali tete. Kwenye utangulizi wake wa takribani dakika nane, alizungumzia mada moja tu: usalama wa kijamii, usambazaji thabiti wa nishati, umadhubuti - kwa sababu hili linamaanisha: "Hutatembea peke yako!" Nyimbo ya timu ya soka ya England ambayo Scholz ameigeuza kuwa kaulimbiu yake. Yeye, ni kansela kutoka chama cha usoshalisti wa wastani - SPD.

Christoph StrackPicha: DW

Wasiwasi juu ya usambazaji thabiti wa nishati kwa Wajerumani katika majira ya kipupwe yajayo kwa kweli upo. Lakini Scholz anajitahidi kujitenga na awamu zilizopita za serikali ambazo alikuwa waziri wa kazi na masuala ya kijamii, waziri wa fedha na naibu kansela, na anazituhumu awamu hizo kwa kuyaangalia mambo kijuujuu.

Scholz anataka taswira moja tu kuhusu yeye isalie vichwani mwa watu. Kwamba yeye ni baba huruma, ambaye chini ya uongozi wake, kima cha chini cha mshahara kinapanda na hivyo wenye kipato kidogo wanapata utulivu wa maisha, jambo linaloashiria dhana na dola yenye ustawi.

Bingwa wa mchezo

Scholz anaujuwa mchezo halisi wa mikutano ya waandishi wa habari, ambayo sasa imejaa matarajio. Matarajio ambayo wao wanasiasa kama walivyo wanahabari kamwe hawawezi kuyakidhi. Na anaucheza mchezo huu kwa kujiamini kabisa.

La mwisho, anajipa yeye na chama chake uhakika kwamba anajinasibisha na wananchi. Hii ndivyo ilivyo kwenye suala kubwa la sera ya nje katika zama hizi, yaani jibu na namna ya kushughulika na mashambulizi ya Urusi kwa Ukraine.

Kwa uwazi kabisa na kwa hali ya kushangaza, Kansela Scholz anamtanganishaPutinwa Urusi na Warusi walioko vitani na Warusi wengine kwa ujumla. 

"Hivi ni vita vya Putin", anasema, akiongeza kwamba rais huyo wa Urusi ndiye aliyeamua kuwa vita hivi viwepo. Vita ambavyo vinavunja kanuni zote.

Lakini alipoulizwa, Scholz hakutaka kumuita Putin waziwazi kuwa ni mhalifu wa kivita wala kukubali kuwa Warusi wote kwa ujumla wao wanawajibika kwa uvunjaji huu mkubwa wa sheria za kimataifa.