1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yawafurusha waandishi wa habari wa nje

Zainab Aziz Mhariri: Josephat Charo
21 Februari 2020

Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka kama 30, China imewafukuza waandishi kadhaa wa nje. Hatua hiyo ni ishara ya mapungufu katika kushughulikia virusi vya Corona. Anasema mwandishi wa DW Philipp Bilsky.

China Coronavirus Klinik in Wuhan
Picha: Getty Images/AFP

Mnamo Februari 19, China iliwaamuru waandishi wa habari watatu wa jarida la Marekani Wall Street Journal (WSJ) kuondoka nchini baada ya jarida hilo kuchapisha habari ambazo kichwa chake cha habari kilikuwa "China ndiye mgonjwa kabisa wa bara Asia," makala hiyo iliandikwa na mmoja wa waandishi wanaochangia kwenye ukurasa wa maoni kwenye gazeti hilo.

Katika makala hiyo ya maoni, mwandishi alikosoa usimamizi duni katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa mafua yanayosababishwa na virusi vya Corona ambavyo vimetikisa ujasiri na imani ndani ya chama cha Kikomunisti cha China nchini humo na nje ya nchi hiyo.

Mwandishi aliendelea kueleza kwenye maoni yake kuhusu virusi hivyo au mlipuko mkubwa wa virusi hivyo hapo baadaye na jinsi unavyoweza kuathiri uchumi wa ulimwengu mzima.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje ya China aliunga mkono kufukuzwa kwa waandishi wa jarida la Wall Street kwa kutolea mfano maneno yaliyotumika kwenye kichwa cha maoni yaliyoandikwa.

Alisema kwamba kichwa cha habari cha makala hayo kilikuwa kimelemea katika misingi ya ubaguzi na kwa kuilezea China kuwa ndio mgonjwa wa bara Asia inaifanya nchi hiyo kukumbuka ilivyokandamizwa na kunyonywa na wakoloni wa nchi za Magharibi. Amesisitiza kwamba inapasa kuelewa kuwa serikali ya China na raia wengi wana hisia kali kuhusiana na kumbukumbu hii ya kihistoria.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Geng Shuang.Picha: picture-alliance/newscom/UPI Photo/S. Shaver

Mwandishi wa DW anasema kweli kichwa cha habari cha makala hiyo kinaweza kuzingatiwa kuwa kisichofaa kwa kuzingatia tatizo la afya lililopo sasa lakini hatua ya kufukuzwa kwa waandishi hatua hiyo si sawa kabisa.

Kwa kuongezea, serikali ya China ikiwa mtu ataamini maneno ya msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje itauwa ni dhahiri kufukuzwa huko sio tu kwa ajili ya habari iliyochapishwa, lakini pia inahusu kuukosoa usimamizi wa serikali ya China katika kukabiliana na migogoro kwa jumla. Serikali ya China inaamini kwamba makala hiyo imedharau moja kwa moja juhudi zake.

Hali ya serikali ya China kuwa na wasiwasi inaweza kuwa ni kutokana na matokeo ya kukosolewa kwenye wavuti ya ndani ya nchi hiyo jinsi inavyokabiliana na virusi vya Corona, haswa baada ya kifo cha daktari Li Wenliang ambaye alikuwa ni mmoja kati ya madaktari  wa kwanza waliogundua virusi hivyo hatari.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo akijibu juu ya kufukuzwa kwa waandishi hao wa habari amesema: Nchi zilizokomaa na zinazowajibika ila shaka zinaelewa kuwa vyombo vya habari huru vinaripoti ukweli wa mambo na pia ni muhimu kwa wandishi kutoa maoni yao. Pompeo amesema hatua sahihi ni kuwasilisha hoja zinazopinga taarifa na sio kuwazuia wanahabari kutoa maoni au kuripoti.

Cha kushangaza ni kwamba wasomaji wa taarifa mbali mbali  nchini China hawawezi kutoa mawazo yao wenyewe juu ya kile wanachofikiria kuhusiana na maoni aliyoandika mwandishi wa jarida la WSJ na iwapo wanapaswa kukasirika kutokana na hoja hiyo kwa sababu jarida la hilo limezuiwa nchini China kwa muda mrefu sasa.

Chanzo:/ https://p.dw.com/p/3Y30v

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW