1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni: Kumfungia Trump mitandao ya kijamii haitoshi

11 Januari 2021

Mitandao ya Facebook na Twitter imemfungia Rais wa Marekani Donald Trump. Hii ni hatua muhimu kwa kampuni ambazo zinajaribu kujisafisha. Mhariri Mkuu wa DW Manuela Kasper-Claridge, anasema, hatustahili kuwapa nafasi.

Symbolbild I BigTech I Social Media
Picha: Jakub Porzycki/NurPhoto/picture alliance

Lakini Mhariri Mkuu wa DW Manuela Kasper-Claridge katika maoni yake, anasema, hatustahili kuwapa nafasi wafanye hivyo.

Rais wa Marekani Donald Trump ambaye anaweza kufananishwa na Goliath wa mitandao ya kijamii, ameangushwa, ingawa hajaangushwa na mshindani mdogo. Ameangushwa na Twitter, Facebook, Google, Amazon na Apple ambao wametosheka na uchochezi wake. Wameweka wazi kwamba wao ndio watakaoamua yule atakayetumia mitandao hiyo na kivipi na sasa wamemfungia mtumiaji wao maarufu kabisa.

Sasa wafuasi wake milioni 88 wa Twitter na wengine milioni 35 wa Facebook, hawatopata taarifa zake ambazo wakati mwengine ni za ubaguzi wa rangi na hatari. Rais huyo amefungiwa kabisa. Trump alitumia kurasa zake za mitandao hiyo kama silaha kwa wale wanaompinga.

Hatimaye kuna amani baada ya Trump kufungiwa

Maneno ya uchochezi na taarifa za uongo ndiyo mambo yaliyompa umaarufu kwenye kitandao hiyo. Matokeo ya maneno aliyokuwa akiyaandika katika Twitter yalionekana wakati wa uvamizi katika jengo la bunge la Capitol huko Washington.

Rais wa Marekani Donald TrumpPicha: Donald J. Trump via Twitter/REUTERS

Lakini sasa wengi wanasema hatimaye kuna amani na mimi pia ninaona ni afueni, lakini ni kwa muda tu, kwasababu ukitaka uhuru wa kujieleza ni sharti uukubali uhuru huo wa kujieleza. Ni jambo linalonipa wasiwasi kwamba kundi dogo la watu linaweza kuamua kuufunga mlango wa majukwaa muhimu zaidi ya mawasiliano duniani.

Hebu tuweni wazi hapa: Hatuzungumzii uchochezi au taarifa za uongo tu. Taarifa hizi zinastahili kutambuliwa na kufutwa mitandaoni, hilo ndilo jukumu la wanaoendesha mitandao hii, jukumu ambalo hivi majuzi wamekiri ni lao na wameanza kulitekeleza.

Mnamo mwezi Mei ndiyo kwa mara ya kwanza Twitter walimpa onyo Trump kutokana na taarifa alizokuwa ameziandika Twitter na kutokea wakati huo, taarifa nyingi zaidi alizokuwa akiandika kwenye Twitter, zilikuwa zinafutwa au anapewa onyo. Kila mmoja alianza kuona jinsi taarifa za Donald Trump zilivyokuwa hatari sasa. Hicho kilikuwa kitu kizuri.

Twitter na Facebook wafute ujumbe wa chuki na uchochezi mitandaoni

Lakini kuufungia ukurasa wake wa mtandao kijamii kwa sasa ni rahisi sana ila waendeshaji wa mitandao hiyo wanashindwa na jukumu lao kwani mamilioni kwa mamilioni ya watu wanaandika taarifa za uongo, chuki na propaganda kwenye mitandao.

Mhariri Mkuu wa DW Manuel Kasper-ClaridgePicha: DW

Kutokana na hili Twitter na Facebook wanastahili kutekeleza jukumu lao kikamilifu kwa kufuta kila mara ujumbe wenye chuki na kutambua na kufahamisha watu kuhusiana na ripoti za uongo.

Kufunga kurasa za mitandao kama vile alivyofanyiwa Trump, sio suluhisho ila njia ya kuwafanya watumizi wakubwa wa mitandao kutotimiza jukumu lao la kuitumia vyema mitandao hiyo.