1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni: Merkel na Putin - Si marafiki lakini ni washirika

Sekione Kitojo
13 Januari 2020

Katika mazungumzo mjini Moscow, kansela wa Ujerumani Angela Merkel alijadili pamoja na rais wa Urusi Putin pamoja na mambo mengine hali katika eneo tete la mizozo la Mashariki ya Kati. Viongozi hao walitoa ushauri.

Russland Deutschland Merkel und Putin Treffen
Picha: picture-alliance/dpa/TASS/M. Metzel

Katika uhariri ulioandikwa  na  mwandishi  wa DW Juri Rescheto, anajiuliza iwapo  Urusi  na  Umoja  wa  Ulaya  sasa  zinaelekea  kukaribiana zaidi. Hili mhariri  anaandika  kuwa  lingekuwa  jambo  zuri kutokana na  hali  ilivyo  katika  mashariki  ya  kati. 

Nchini Urusi  kuna  msemo usemao, "Niambie, nani  ni  adui yako , na  nitakwambia  wewe  ni  nani." Angela  Merkel  na  Vladimir Putin si marafiki kabisa, lakini  ni  washirika, katika  uchumi  na  siasa. Pamoja  na  vikwazo  vilivyowekwa  dhidi  ya  Urusi  pamoja  na mauaji  ya  raia  wa  Urusi  mjini  Berlin, pamoja  na  kuliingiza  katika himaya  yake  eneo  la  Crimea  na  vita  katika  eneo  la  Donbass nchini  Ukraine, pamoja na  tofauti  za  kisiasa , viongozi  hao wanakaribiana  kuliko viongozi wengine. Merkel  anamhitaji  Putin. Ulaya  inaihitaji Urusi.

Iwapo mtu anapenda  ama la, ukweli  ni  kwamba  ushawishi  wa Urusi  katika  mashariki  ya  kati ni  mkubwa. Hususan  kutokana  na hali ya  kuwa  na  ombwe la uongozi, ambalo  Marekani  imeliacha, Urusi imesongambele  katika  hilo  katika  eneo  lote.

Nchini  Libya, ambako  kuna hatari ya  vita  vya  wenyewe  kwa wenyewe kupamba  moto na  ambako  kunaweza  kutarajiwa mmiminiko  mwingine  wa  wakimbizi  kuelekea  Ulaya.

Mwandishi wa DW mjini Moscow Juri ReschetoPicha: DW/Juri Rescheto

Nchini  Syria , ambako  Putin  amesema  kuwa  yuko  upande wa kiongozi wa  nchi  hiyo Bashar al-Assad kijeshi. Nchini Iran , rais huyo wa  Urusi  anajionesha wazi   kuwa ni mshirika.

Putin  anaweza  kutumika  katika  utatuaji  wa  mizozo  yote  hii. Na hilo  analifahamu.  Na anaamini  kuwa  ni  mtu  muhimu , kama anavyoonekana  katika  medani  ya  kimataifa, kwamba  haiwezekani kumuachia  yote  haya  peke  yake, kwamba  Urusi  nchini  Syria  sio mchochezi wa  vita , badala  yake  anachukuliwa  kama  ni mpatanishi  wa  amani. Na  hatimaye  vikwazo vya  mataifa  ya magharibi  vinaweza  kulegezwa  siku za  baadaye.

Swali  baada  ya  mazungumzo  ya  masaa  mawili  mjini  Moscow ni iwapo Ujerumani  iko tayari, kuingia katika ushirikiano  mpya,  ambao utaiweka  nchi hiyo mbali na  Marekani. Tangu  pale Donald Trump kuwaona Merkel  na  Putin  kuwa ni  maadui, katika  masuala  ya uchumi  na  siasa, Ujerumani  inahitaji kwa  udi  na  uvumba  gesi kutoka  Urusi kupitia  mradi  mkubwa  wa  bomba  la  Nord Stream 2, Marekani  inataka  kuzuwia  mradi  huo kwa  njia  yoyote  ile. Ndio sababu  mawaziri  wa  mambo  ya  kigeni  wa  Urusi na Ujerumani wamezungumzia  tofauti  kuhusu kuuwawa kwa  jenerali  wa  Iran Qassem Soleimani  na  Marekani.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW