1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni: Mshindi ni jumuiya ya Umoja wa Ulaya

26 Julai 2018

Rais wa Marekani Donald Trump atayanadi makubaliano ya muda aliyofikia na Umoja wa Ulaya kuwa ni mafanikio yake lakini mwandishi wa DW Carsten von Nahmen anasema makubaliano hayo ni mafanikio ya Umoja wa Ulaya.

USA Washington Jean-Claude Juncker, Präsident EU-Kommission & Donald Trump
Picha: Reuters/J. Roberts

Ni vipi alivyoweza kufanikiwa bwana Jean Claude Juncker? Rais huyo wa halmashauri ya Ulaya amepata mafanikio makubwa zaidi kuliko alivyotarajia. Mazungumzo yalikuwa juu ya hatua mpya - hatua  mpya ya urafiki wa karibu baina ya Marekani na Umoja wa Ulaya kwa lengo la kuondoa ushuru na vizingiti vingine katika biashara. Na hayo yote yamefikiwa katika muda  wa wiki chake tu. Kabla ya hapo rais Donald Trump alikuwa anatoa kauli kali dhidi ya Umoja wa Ulaya na hasa dhidi ya Ujerumani.

Kabla ya mazungumzo kati ya Trump na rais wa halmashauri ya Ulaya kufanyika matarajio yalikuwa kattika kiwango cha chini. Mnamo wiki zilizopita alichosema na alichoandika Trump kwenye  mtandao wa Twitter zilikuwa shutuma dhidi ya Umoja wa Ulaya na madai kwamba jumuiya hiyo  inaendesha biashara isiyokuwa ya haki.

Rais wa Marekani Donald TrumpPicha: Getty Images/AFP/S. Loeb

Trump aliuita Umoja wa Ulaya kuwa ni adui wa Marekani na akaamua kuyatoza ushuru mkubwa magari ya nchi za Ulaya yanayouzwa nchini mwake. Hata siku moja tu kabla ya rais wa halmashauri  ya Ulaya Juncker kwenda Marekani hakuna yeyote kwenye Umoja wa Ulaya aliyetarajia kuwa mafanikio yatapatikana. Bwana Juncker amewasili nchini Marekani wakati ambapo upinzani dhidi ya sera za biashara za Trump umeanza kuimarika.

Pamoja na msimamo thabiti wa washirika wa Marekani wa kupinga sera za Trump, ndani ya chama chake cha Republican pia wamejitokeza watu wa kumpinga.Vyama vya wafanya biashara na  wakulima wa Marekani pia wamejitokeza kuzipinga sera za biashara za rais wao. Pande hizo zilihesabika kuwa nguzo ya kumuunga mkono rais Trump.Lakini sasa zimeanza kuona athari za siasa ya mvutano inayoendeshwa katika biashara dhidi ya Japan,China, Mexico na hata dhidi ya Umoja wa Ulaya.

Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Jean-Claude JunckerPicha: Getty Images/K. Dietsch

Hata hivyo rais Trump anayetetea sera ya Marekani kwanza ametambua kwamba wakati umefika wa kufanya mabadiliko. Ni vizuri kufuata sera ya ushirikiano badala ya mvutano, angalau kwa sasa tu ili kuinadi sera hiyo kwa watu wake wanaomuunga mkono kuwa ni ushindi, lakini ukweli ni kwamba makubaliano yaliyofikiwa ni ushindi kwa nchi za Umoja wa Ulaya.

Nchi za Umoja wa Ulaya ziliamua kusimama pamoja wakati Trump alipojaribu kutoa vitisho ili zisalimu amri. Umoja wa Ulaya ulipambana mashinikizo ya Trump kwa kutoa mashinikizo yao na kamwe haukusalimu amri hata pale ambapo rais Trump alitishia kuvitoza ushuru mkubwa viwanda vya magari vya nchi za Umoja wa Ulaya .     

Ni kweli kwamba mwafaka ulihitajika. Sasa nchi za Umoja wa Ulaya zitanunua gesi zaidi pamoja na maharage ya soya na pia zitaagiza bidhaa zaidi za kilimo kutoka Marekani.

Mwandishi: Zainab Aziz/Carsten von Nahmen

Mhariri: Yusuf Saumu

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW