1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni: Mwaka mmoja wa Scholz uongozini, sifa zapiku ukosoaji

8 Desemba 2022

Serikali ya mseto ya Ujerumani imehudumu kwa mwaka mmoja sasa. Licha ya ukosoaji mwingi katika mwaka wao wa kwanza, hakuna mapungufu makubwa ya kutajwa. Ni kulingana na maoni ya Marcel Fürstenau.

Deutschland | Bundeskanzer Olaf Scholz bei der Kabinettssitzung
Picha: Clemens Bilan/EPA-EFE

Mtunzi mmoja maarufu wa mashairi nchini Ujerumani Johann Wolfgang aliwahi kusema dhana zote ni rangi ya jivu yaani hazibainiki moja kwa moja. Kansela Olaf Scholz na serikali yake ya muungano wamethibitisha busara iliyoko kwenye kauli hiyo.

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz yuko Saudi Arabia kusaka nishati kwenye nchi za Ghuba

Serikali ya muungano haikuwa na muda wa kutosha kujiweka sawa ilipochukua hatamu za uongozi kutoka kwa serikali iliyotangulia.

Ukweli ni kwamba muungano huo umekuwa ukitawala katika hali ya dharura tangu siku yake ya 79 ya muhula wake madarakani.

Wakati wa mabadiliko

Siku hiyo Februari 24, Urusi iliivamia Ukraine. Lakini katika bunge la Ujerumani, Olaf Scholz, kansela wa kwanza wa chama cha Social Democratic baada ya miaka 16 ya utawala wa Angela Merkel aliyekuwa wa chama cha CDU, alitangaza kuwa umewadia wakati wa mabadiliko.

Rais wa Ujerumani asema taifa linakabiliwa na nyakati ngumu

Mwandishi wa DW Marcel FürstenauPicha: DW

Ni jambo la kweli, sahihi na linaloeleweka kwa rais wa Urusi Vladimir Putin ameanzisha uchokozi kwa kuivamia jirani yake, hali inayoathiri Urusi, Ukraine, Ujerumani na ulimwengu kwa jumla. Scholz aliutaja uvamizi wa Urusi nchini Ukraine kuwa ubeberu.

Kulingana na makubaliano ya muungano huo, serikali ya Ujerumani inajitizama kama muungano wa uhuru, haki au sheria na uendelevu. Kutimiza hayo wakati wa vita na tena baada ya janga la Covid, imekuwa kazi ngumu ambayo serikali ya Scholz imefanikiwa kutekeleza licha ya ukosoaji.

Kuonesha sifa za uongozi wakati wa shida

Kwa mfano tofauti ilipoibuka kuhusu kurefusha muda wa mitambo ya nishati ya nyuklia ambayo iliratibiwa kufungwa, kansela alijitokeza na kutoa mwelekeo kama kiongozi.

Ukraine yapokea mfumo wa ulinzi wa makombora wa Ujerumani

Ujerumani imepata sifa kuhusu sera za kigeni na usalama. Haijalishi watu watahisi vipi kuhusu matumizi makubwa ya jeshi kifedha ambayo yalitangazwa na Scholz, kwa mujibu wa mfumo wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO, kwani hiyo inaashiria kutegemewa na mshikamano.

Waziri Robert Habeck wa Uchumi nchini Ujerumani (Kulia) na mwenzake wa Mambo ya Nje Annalena Baerbock.Picha: Michael Sohn/ASSOCIATED PRESS/picture alliance

Scholz anastahili kupongezwa kwa kukataa iliyokuwa miito ya mara kwa mara ya kuipa Ukraine silaha zaidi. Kwa wakati huo huo, hakuna awezaye kusema kuwa chini ya uongozi wake, Ujerumani haijayumba kusaidia pale ambapo silaha zinahitajika.

Mipango ya ruzuku

Ilimradi kansela na serikali yake wanashirikiana kimataifa, wapo katika njia sawa. Kuhusu vita na amani, hali yake ya kutoa hotuba kwa utulivu, humweka kuwa tofauti na kejeli kwa wengine ambao diplomasia imekuwa neno geni kwao.

Licha ya vita nchini Ukraine, serikali ya muungano nchini Ujerumani ina mengi ya kujivunia. Zaidi ya yote ni miradi mingi ya misaada kusaidia raia kutokana na ongezeko la bei ya nishati pamoja na mfumuko wa bei. Tayari zaidi ya euro bilioni 200 zimetumika katika mipango ya ruzuku kuwasaidia raia na vilevile kusaidia uchumi.

Maoni haya yaliandikwa mwanzo kwa lugha ya Kijerumani.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW