1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufalme wa Uingereza wailinda nchi dhidi ya kusambaratika

19 Septemba 2022

Falsafa ya serikali ya Jamhuri imeibuka tena baada ya kifo cha Malkia Elizabeth. Mwandishi wa DW Sertan Sanderson anasema ufalme unahitajika zaidi hivi sasa katika taifa hilo linalokabiliwa na kitisho cha kusambaratika.

England Edinburgh | Gegner der britischen Monarchie
Picha: Jane Barlow/PA Wire/dpa/picture alliance

Ni dhahiri kwamba Uingereza imepoteza aina ya kiongozi ambaye ni nadra kumpata siku hizi: Mwanamke ambaye kwa miongo kadhaa ameshawishi matukio ya kisiasa kama mkuu wa nchi: mwanamke ambaye amebainisha nguvu ya diplomasia.

Malkia Elizabeth II ametembelea zaidi ya mataifa 100 wakati wa uhai wake, na kwa kila mkono alioushika, alitoa tabasamu kwa viongozi wote wa Jumuiya ya Madola katika juhudi za kuanza kushughulikia - na kushughulikia tena yaliopita.

Soma pia: Ulimwengu wamuaga Malkia Elizabeth II

Alisafisha njia kwa usasa na ufalme kukutana na alijitolea kwa dhati, moyo na heshima, wakati wote akitafuta kuwa nguzo ya ujenzi wa taifa, wakati ambapo ulimwengu wote wa baada ya ukoloni ukipitia mabadiliko makubwa.

Malkia Elizabeth II enzi za uhai wake.Picha: Chris Radburn/dpa/picture alliance

Ushahidi wa kifalme

Wakati kila koloni likitangaza uhuru wake, Uingereza iliporomoka kutoka himaya hadi chini ya mpatanishi. Pamoja na hayo, Malkia alikuwa na wakati mzuri wa utawala, akisimamia lundo la mabadiliko ya kijamii nyumbani na nje kwa miaka 70.

Wakati himaya kubwa ya Uingereza ikiingia katika miaka yake ya mwisho ya ubeberu, aliweka wazi vipengeee zaidi na zaidi vya maisha yake kwa umma, wakati ambapo nafasi ya ugeni wa himaya ilichukuliwa na familia yake mwenyewe ili kuufanya umma uendelee kuuamini ufalme.

Kamera za televisheni ziliingia katika kumbi za kasri la Buckingham, na kuuruhusu umma kujionea ulimwengu wa fursa ambao ulikuwa umetota katika siri kwa karne kadhaa.

Soma pia: Viongozi wa ulimwengu waanza kukusanyika nchini Uingereza kwa ajili ya kuhudhuria mazishi ya Malkia Elizabeth wa ll.

Baadae alikubali kulipa kodi juu ya mapato yake binafsi, na wakati makaazi yake pendwa ya Kasri la Windsor yalipotekelezwa mnamo mwaka 1992, aliamua kutafuta njia mpya za kufadhili ukarabati kutoka mfukoni mwake.

Sertan Sanderson ni ripota wa DW mjini London.

Inaweza kuwa vigumu kusema kwamba aligeuka mmoja wetu, lakini alau alifanikiwa katika kuonesha kuwa hakuwa mtakatifu kuliko wewe.

Kutunza amani

Malkia alionesha utofauti na kusawazisha mambo nyumbani, kinyume kabisa na ukosefu wa utawala wa kisiasa nchini Uingereza, ambayo imeshuhudia mabaraza dhaifu ya mawaziri wakuu wanne katika kipindi cha muongo mmoja pekee uliopita.

Miaka hiyo 10 iligubikwa na migawanyiko ya kijamii na ugomvi chini ya kila mmoja wa viongozi hao - kuanzia kura ya maoni juu ya uhuru wa Scotland hadi suala la Brexit, na janga la Covid-19. Hata hivyo Malkia alisalia kuwa yule yule wakati wote, akihudumu kama gundi inayoishikilia pamoja Uingereza.

Soma pia: Urusi yalaani kutoalikwa mazishi ya Malkia Elizabeth

Maumivu ya Kifalme

Wakati huo huo, hakuna shaka kwamba yapo masuala ndani ya familia ya kifalme, ambapo baadhi ya wanafamilia wa ukoo wake wameshuhudiwa wakiangukia kwenye kosa moja baada jengine na malumbano ya mara kwa mara miongoni mwa wanafamilia hao.

Lakini matukio hayo ya kuzozana ndani ya familia ya kifalme yanatukumbusha tu namna wanawafalme walivyo binadamu.

Ndiyo, wanaweza kuwa wanaishi katika makasri yaliojengwa kupitia unyonyaji wa sehemu nyingine za dunia. Tunaweza na tunapaswa kuhoji hilo. Na tunaweza pia kuhoji nini maana ya kuwa na ufalme wa kikatiba.

Soma pia: Viongozi wa Afrika waomboleza kifo cha Malkia Elizabeth II

Lakini tunapaswa kukumbuka pia kwamba taji linalotoa hifadhi kwa utajiri wa Afrika ulioporwa, pia linawakilisha maridhiano, uanzishwaji upya wa mahusiano ya kimataifa na hata malipo ya fidia.

Mfalme wa Uingereza Charles III na wanafamilia ya Kifalme wakisindikiza jeneza la Malkia Elizabeth II ndani ya Kasri la Windsor, Septemba 19, 2022.Picha: Adrian Dennis/AFP

Linawakilisha miongo kadhaa ya juhudi za kurekebisha makosa ya karne kadhaa, na kutekeleza mabadiliko pasina uasi.

Wito wa kikazi

Wale wanaotumia kifo cha Malkia kama jukwaa la kuitisha mapinduzi wanaokena kusahau namna gani mabadiliko yametokea katika wakati wa Malkia Elizabeth, na namna alivyomudu mabadiliko hayo kama mkuu wa nchi, kiongozi wa Jumuya ya Madola, mlinzi wa imani na mama wa ukoo wa familia.

Alipotawazwa mwaka 1952, Malkia alitangazwa kuwa mtumishi wa Mungu: Naweza kuhoji kwamba ameweza pekee yake kubadilisha tafisiri ya ufalme. Shukuran kwa dhamira yake isiyoyumba, wafalme wa baadae wataweza kutekeleza majukumu yao kama watumishi wa watu.

Waingereza wauaga mwili wa Malkia Elisabeth II

01:39

This browser does not support the video element.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW