1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni : Septemba 11 sura mpya kwa historia ya dunia

11 Septemba 2016

Mashambulizi ya Kituo cha Biashara Duniani na Wizara ya Ulinzi nchini Marekani hapo Septemba 11 2001 yalikuwa ni tukio la kihistoria lisilokuwa na mfano ambapo Miodrag Soric anasema hadi hii leo linaendelea kukereketa.

Picha: AP

Kufuatia kuanguka kwa Ukuta wa Berlin mataifa ya mgharibi yalipata kupumuwa kidogo. Mtaalamu mashuhuri wa siasa Francis Fukuyama alitangaza huo ulikuwa ni "mwisho wa historia" na wanasiasa wakafaidika na matunda ya amani.Marekani ikajipachika kifuani mwake nishani ya maguvu. Waliokuwa maadui zamani katika kundi la mataifa ya magharibi ilibidi wafuate sheria ya mchezo venginevyo yanawekwa kando.


Hata hivyo baada ya kumalizika kwa Vita Baridi Marekani haikuonyesha shauku ya kutaka kusarifu mambo kama ilivyokuwa imeonyesha mara baada ya kumalizika kwa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia ambapo Jumuiya ya Kujihami ya Mataifa ya magharibi NATO ikaanzishwa,Umoja wa Mataifsa ukaundwa na Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa yaani mfumo mpya duniani.

Wakati Bill Clinton alipoingia madarakani katika miaka ya tisini aliendelea kubakia kama mwanasiasa wa jimbo hata baada ya kuhamia Ikulu ya Marekani kutoka jimbo la Arkansas.Kulikuwa hakuna muundo mpya wa usalama eneo la kaskazini mwa dunia,hakuna juhudi za kutosha kuupiga vita umaskini eneo la kusini,suala la kuhifadhi mazingira ndo kabisa halikutiliwa sana maanani na hakuna suala la amani ya kudumu Mashariki ya Kati.

Shambulio la Septemba 11 ambalo ni la kwanza kufanyika katika ardhi ya Marekani tokea lile la Pearl Habour limekuja bila ya kutegemewa kabisa.

Miodrag Soric wa DW.Picha: DW/Stefan Czimmek

Wamarekani walipata pigo hilo wakati huwakujiandaa lilimewachanganya akili watu wengi hadi hii leo.Siku hiyo inatowa mwangi hadi hii leo na kama Mkurugenzi Mkuu wa Shrika la Ujasusi la Marekani CIA Generali David Petraus alivyoiambia DW kwa uchungu kwamba "Mapambano dhidi ya ugaidi yatadumu kwa vizazi vingi."

Katika siku ziliofuatia shambulio hilo la Septemba 11 hakuna mtu aliyekuwa na mtizamo huo. Suala muhimu wakati huo lilikuwa namna ya kuizuwiya dunia isitumbukie katika mdororo wa kiuchumi. Mabenki Kuu ya Nchi yalifunguwa milango na kukatokea ulanguzi wa fedha.Kwanza kulikuwa na mafanikio halafu masoko ya hisa yakawa yanazidi kuporomoka.

Lakini miaka michache baadae sio mabenki wala wateja hakuna aliyejuwa nini cha kufanya na fedha hizo zilizokuwa zikipatikana kwa urahisi.Mtu yoyote nchini Marekani aliyekuwa akiweza kwa kiasi fulani kulitaja jina lake kwa usahihi alikuwa akiweza kupatiwa mkopo. Mtu alikuwa akiweza kujinunulia nyumba iwe Florida au mahala kwengineko na mara nyingi hata wale wasiomudu.

Mwaka 2008 uchumi ukaja ukaanguka na Marekani ikalazimika kuchapisha fedha zaidi utaratibu ambao unaendelea hadi hii leo. Wanasiasa wakaliweka kando suala la matatizo ya kimuundo na wakati huo huo hali ya kiwango cha maisha ikashuka na kuwaathiri hata tabaka la wafanyakazi.

Mpango wa Osama bin Laden ukaonekana kufanya kazi kwani alichokuwa akikitaka sio kuishina Marekani kijeshi bali kuifilisi kifedha nchi hiyo.

Rais Obama alijifunza kutokana na makosa waliofanya watangulizi wake .Aidha alipunguza sana vikosi vya Marekani vilioko nje au hata kuviondowa kabisa.Hata baada ya kujitowa Iraq kumegharimu mabilioni ya fedha za walipa kodi wa Marekani.

Kutahitajika umakini kidogo kutabiri kilioko usoni.Jambo moja la uhakika ni kwamba kuwa na usalama kwa wote baada ya shambulio la Septemba 11 ni kwa Marekani kuuwekea vizingiti uhuru wa faragha na kuzitolea muhanga haki za binaadamu au sheria ya kimataifa.

Septemba 11 ilikuwa sio alama ya kihistoria tu bali ni siku ilioweka dhamira ya msingi kwa kuanza kwa karne ya kupambana na ugaidi.

Mwandishi :Miodrag Soric/ Mohamed Dahman/

Mhariri . Saumu Yusuf

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW