1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni: Siku ya wanawake duniani wanawake wanapaswa kujiamini

Sekione Kitojo
9 Machi 2020

Wanawake katika  enzi hizi za mabadiliko ya mfumo wa  kisiasa  ni wachache wanaofanikiwa na kwamba  mabadiliko hayo hayajachukuliwa kama kitu cha kawaida.

Argentinien Proteste in Buenos Aires zum Internationalen Frauentag
wanawake wakifanya maandamano katika siku ya wanawake duniani mjini Buenos Aires , ArgentinaPicha: Reuters/M. Baglietto

Lakini, nje ya  mfumo wa siasa  za kibunge  inaonekana  wanawake wanapata  nguvu  zaidi, kama anavyoeleza Anja Brockmann  katika uhariri  wake kuhusu siku ya  kimataifa  ya  wanawake, hapo jana.

Ukiangalia  hali ya maendeleo ya  wanawake  duniani , unaweza kuingiwa  na  mashaka  kidogo. Nchini  Marekani  mwaka huu  pia hakutakuwa  na  mwanamke  katika  uongozi wa  juu  kabisa  nchini humo. Nchini  Afghanistan wanawake  wanakabiliwa  na  kitisho  cha kurudi  nyuma  katika  enzi  za  giza  kutokana  na  mkataba  uliotiwa saini  baina ya Marekani na  kundi  la  Taliban. Na  katika  bara  la Ulaya  mpango  wa  rais  wa  halmashauri  ya  Umoja  wa  Ulaya Ursula  von der Leyen , kutaka  halmashauri  yake iwe na usawa  wa wanawake na  wanaume  unapata  upinzani  kutoka  kwa  viongozi wa  nchi  wanaume.

Wanawake  kupata uongozi wa  kisiasa  duniani  kote  bado linabakia  kuwa  suala  la  nadra  sana. Ni  nadra  sana,  ambapo ikitokea   basi vyombo  vya  habari  huiona  ni  habari  kubwa  sana, kama  ilivyotokea  hivi  karibuni  kwa  waziri  mkuu  wa  Finland Sanna Marin, ambaye sio tu  mwanamke, lakini  pia  ni  kijana na kwa  hiyo  ni  hali  ambayo  si  ya  kawaida mara mbili. Katika mabunge  mengi  humu  duniani , wabunge  wanawake  wamo  katika kifungu  cha  idadi  ya wachache, licha  ya  kuwa  wazo  la  kuwa  na demokrasia  ya  bunge  kama  kioo cha  jamii  inapingana  nayo.

Mhariri : Anja Brockmann wa DWPicha: DW

Na  bila  shaka , hata mwanamke  mwenye madaraka   makubwa duniani, Angela  Merkel , katika  nchi  yake  Ujerumani ameshindwa kupata  nguvu  ya  kusema na  kuwasaidia   wanawake  katika chama chake kuweka mfumo  wa  kuwa  na  kiwango  fulani  cha wanawake  ili  kuwa  na  ushawishi  wa  kutosha. Kwa  hiyo si  ajabu, kwamba  kwa  hivi  sasa  mwanachama  mwezake  katika  chama chake Friedrich Merz, ambaye  angependa  sana  kuwa  kansela  wa Ujerumani, amelalamikia  kuhusu  ubaguzi dhidi  ya  wanaume, akinyooshea  kidole orodha  ya  wagombea  wa  kiti cha  mwenyekiti wa  chama, kwamba  kuna  wanawake  wengi  kuliko  wanaume.

Na  kutokana  na  hali  hiyo, orodha  ilibadilishwa. Hata hivyo kuna wanawake , ambao  hawajiweki  nje  ya  siasa. Wale  ambao hakuna  mwanamume  ambaye  anaweza  kuwapita.  Wanawake kama  Greta Thunberg , ambaye  kitisho cha  maafa  ya  mabadiliko ya  tabia  nchi  ameyaweka  katika  ajenda  ya  kisiasa  duniani. Wanawake  kama  Carola Rackete, ambae  kutokana  na   kazi  yake ya  uokozi  kwa  wahamiaji  wanaosafiri  baharini amepambana  na waziri  wa  mambo  ya  ndani  wa  Italia. Wanawake  kama Emma Gonzalez , ambaye  anapambana   kuimarisha  sheria  ya  umiliki  wa silaha  nchini  Marekani.

Mashujaa  hawa  wapya  wa  kisiasa  ni  vijana, wenye  hasira  na wanasukuma  mambo fulani,  katika  upinzani  nje  ya   mabunge. Ni nguvu  mbadala  dhidi ya  wanaume  kama  Donald Trump, Vladimir Putin  na  Jair  Bolsonaro. Wanataka  kuamsha  hali  fulani, bila  wao kuwa na  madaraka. Na wanajiweka  katika  hatari, hatari  ya kuchukiwa na  wanaume. Hata  hivyo  thamani  ya  majina yao ina leta  matumaini  ya  mwelekeo  mpya  wa  kisiasa. Wanakuwa  kioo cha  wanawake  vijana  duniani kote.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW