1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni: Trump atangaza vita dhidi ya waandishi

12 Januari 2017

Mkutano wa waandishi habari wa Donald Trump ulikuwa tangazo la wazi la vita dhidi ya vyombo vya habari vinavyommkosoa, anasema mwandishi mwandishi wa DW mjini Washington Ines Pohl.

USA Wahlen Reaktionen Medien Zeitungen
Picha: Getty Images/AFP/B. Fathers

Kadiri mammbo yanavyozidi kuvurugika ndivyo inavyozidi kuwa muhimu kurudi hatua nyuma na kutopitwa na yaliyomuhimu. Siku ya Jumatano rais mteule Trump aliitisha mkutano wake wa kwanza na waandishi habari katika nafasi hiyoi. Katika demokrasia, uhuru wa habari ni kitu cha tahamani, kwa sababu wandishi habari ndiyo wawakilishi wa raia katika kuwawajibisha waliopewa dhamana ya uongozi.

Hili linatimizwa kwa upande mmoja kupitia utafiti uliofanywa kwa uangalifu mkubwa, na kwa upande mwingine kupitia maswali magumu kwa mfano wakati wa mikutano ya wandishi habari. mkutano huu ulitangazwa muda mrefu na umekuwa ukiahirishwa mara kwa mara. Kimsingi mkutano huu ulipaswa kuhusu namna bilinea huyo angehakikisha kuwa hatatumia mamlaka yake ya urais kuzinufaisha biashara zake. Swali hili siyo dogo, kwa sababu linamnufaisha moja kwa moja kwa mfano, wakati wanasiasa na waraghibishi wanapolala katika hoteli zake.

Hata katika biashara zake za kimataifa, wengi wana wasiwasi kwamba rais huyo ajaye atachanganya malengo ya kisiasa na kibinafsi, hata kama siyo moja kwa moja, kwa sababu atakuwa na taarifa kuhusu vitu vinavyoathiri mustakabali wa masoko, hivyo kumpa faida ya wazi dhidi ya washindani wake kibiashara.

Mwandishi wa DW mjini Washington Ines Pohl.Picha: DW/R. Oberhammer

Tuhuma nzito mkesha wa mkutano

Bomu liliangushwa katika siku ya mkesha wa mkutano huo, wakati vyombo kadhaa vya habari kikiwemo kituo kikubwa kabisaa cha utangazaji CNN, viliporipoti kwamba, mashirika ya ujasusi ya Urusi yalikuwa na taarifa za siri kumhusu kiongozi huyo ajaye mwenye nguvu zaidi duniani, kibinafsi na kibiashara. Taarifa hizo zilikuwa tayari zimeripotiwa na mashirika ya ujasusi ya Marekani, na sasa, siku chache tu kabla ya kuapishwa Trump, zimeufikia umma. Trump alijibu haraka kupitia ukurasa wake wa twita, akiwaita wandishi kuwa waongo na kuzilinganisha tabia za mashirika ya ujasusi na Ujerumani ya wakati wa manazi.

Hii ni kauli nzito, na inaakisi maajabu inamojikuta jamii ya Wamarekani. Ushirikiano kati ya wanasiasa wa juu na tasnia ya habari huwa mgumu kwa sababu maslahi yao yanakuwa yanakinzana. Hali haikuwa tofauti kwa Obama. Katika historia yakaribuni, hakuna rais alievishirikisha vyombo vya habari kama alivyofanya. Lakini katika kampeni za uchaguzi huu wa karibuni, uhusiano huo umetiliwa sumu katika namna ambayo inataka kutikisa misingi ya taifa hilo. Hii inahusiana zaidi na mfumo wa ushari wa Trump. Na ukweli kwamba ametumia njia mpya za kupasha habari kusambaza madai yasiyohakikiwa, kw amfano kuhusu rekodi yake ya ulipaji kodi au hali ya uchumi wa Marekani.

Maswali muhimu hayakujibiwa

Cha hatari zaidi lakini ni kukosa imani katika kazi ya waandishi habari kulikochochewa na Trump. Haijalishi ni kiasi gani ripoti za ukosoaji zimetafitiwa, anazipuuza kuwa za uongo. Kwa namna hiyo, haiwezakani kufuatilia shughuli za serikali kwa uhakika. Kisichoendana na mtazamo wake wa kidunia, kinakataliwa kama uongo. Hili halimhusu tu Trump hata hivyo. Sauti za upinzani mara nyingi ziko tayari kuamini na kusambaza kila taarifa inayomkosoa rais-mteule. Shutuma kuhusu habari za kizushi wa vyombo vya habari vya kiliberali siyo za uongo wakati wote.

Siku ya Jumatano, Donald Trump amedhihirisha wazi kwamba anapanga kuwashughulikia waandishi habari wakosoaji katika siku zijazo. Alikataa kujibu swali la ripota wa kituo cha CNN, kwa sababu kituo chake kilitangaza ripoti zisizohakikiwa kumhusu.Kiukweli huu haukuwa mkutano wa waandishi. Kilikuwa kidokezo cha kwanza juu ya namna rais huyo mteule anapanga kuwashughulikia wandishi wakosoaji.

Mwandishi: Ines Pohl - DW Washington

Tafsiri: Iddi Ssessanga

Mhariri: Mohammed Khelef

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW