1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni: Uchaguzi Marekani - Trump ahujumu demokrasia

Josephat Charo
4 Novemba 2020

Bado haijawa wazi nani aliyeshinda uchaguzi wa rais Marekani na huenda ikachukua muda kabla kujulikana. Haina maana demokrasia iko hatarini, lakini ni kwamba Wamarekani wengi wanaviona vitendo vya Trump havikubaliki

US Wahl 2020 Donald Trump
Picha: Carlos Barria/REUTERS

Usiku wa uchaguzi umekuwa vile walivyotabiri wataalamu na wachambuzi wengi, angalau katika jambo moja - Hakuna mshindi wa wazi kufikia leo asubuhi. Majimbo muhimu yenye ushawishi mkubwa yakiwemo Michigan, Waisconsin na Pennyslvania bado matokeo hayajakamilika na huenda ikachukua muda kidogo kupata matokeo kamili.

Si jambo la kushangaza kwamba wagombea wote wawili, Donald Trump wa chama cha Rrepublican na Joe Biden wa chama cha Democratic, walifanya kila waliloweza kupuuza hali halisi iiyopo na badala yake kuwapa matumaini wafuasi wao. Biden alijitokeza mapema leo katika jimbo anakotokea la Delaware na kusema tulijua mchakato huu utachukua muda mrefu, akiongeza kuwa anahisi vizuri kuhusu walipo katika kinyang'anyiro cha kura za jopo maalumu la wajumbe ambapo mgombea anahitajika kupata kura 270 kushinda urais.

Mwandishi wa DW Marekani Carler BleikerPicha: privat

Huku mifumo mitatu ikitumika kupiga kura, kwa maana ya watu kupiga kura siku ya uchaguzi, upigaji kura wa mapema katika vituo vya kupigia kura na kupiga kura kwa njia ya posta, mchakato wa kuhesabu kura huenda ukaendelea kwa siku kadhaa. Hii ni sehemu muhimu na halali kabisa katika mchakato wa kidemokrrasia. Kumuona Trump akiueleza mchakato huo kama njia ya wafuasi wa chama cha Democtratic kujaribu kuiba kura, kama alivyoandika katika ukurasa wake wa twita mapema leo bila kutoa ushahidi, halitakiwi kuwa jambo la kushangaza, lakini linaudhi.

Katika hotuba yake leo asubuhi Trump amedai ameshinda katika majimbo kadhaa ambayo kufikia wakati huo yalikuwa bado hayajahesabu kura za kutosha kuweza kubaini nani aliyeshinda. Alitaja hasa anaongoza jimbo la Pennsylvannia, bila kuzungumzia kuzingatia kura zipi zingali bado zinasubiri kuhesabiwa. Kura nyingi ambazo bado hazijahesabiwa ni zile zilizopigwa kwa njia ya posta, ambazo wataalamu wanachukulia wafuasi wa chama cha Democratic walipiga kura nyingi kuliko wale wa chama cha Republican. Kwa hiyo Trump hangetaka kura hizo zihesabiwe. Lakini hii pia ina maana wanachama wa chama cha Democratic hawatakiwi kukata tamaa - Trump anaweza kuwa anaongoza katika majimbo mengi ambayo bado mshindi hajapatikana, lakini idadi kubwa ya kura ambazo bado hazijahesabiwa huenda zikamwendea Biden.

Kwa maneno mengine, huku hali ikionekana kama marudio ya yale yaliyotokea katika uchaguzi wa mwaka 2016, bado kinyanganyiro hakijafika mwisho. Lakini hatua ya Trump kutangaza ushindi, kuuita mchakato wa kuhesabu kura kuwa wizi mkubwa na kutangaza kwamba atalifikisha suala hilo mbele ya mahakama ya juu kabisa ya Marekani, inaonyesha kutojali kabisa jinsi kura zinavyohesabiwa katika taifa linalozongwa na changamoto ya janga la corona mwaka huu 2020.

Trump alijitangaza mapema kuwa mshindi Jumatano asubuhi alipojitokeza katika IkuluPicha: Mandel Ngan/AFP/Getty Images

Sio Wamarekani wengi waliokerwa na vitendo vya Trump

Waliberali wengi Wamarekani walikuwa na matumai ya ushindi wa wazi wa Biden, lakini sio mnyukano wa kukabana koo kwa karibu namna hii. Hasa ikizingatiwa kwamba mgombea wao alishindana na rais aliyetaka kuwapiga marufuku Waislamu wasiingie Marekani, aliyewatenganisha watoto wa wahamiaji na wazazi wao katika mpaka wa kusini wa Marekani, aliyetoa kauli za kibaguzi dhidi ya wabunge wanawake katika bunge la Marekani, aliyezongwa na mchakato wa kutaka kumfungulia mashitaka kwa kujaribu kuipa Ukraine msaada wa kijeshi ili imsaidie kumchunguza mpinzani wake, rais ambaye ambaye katika uongozi wake watu zaidi ya robo milioni wamekufa mpaka sasa kutokana na ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na virusi vya corona....orodha inaendelea na kuendelea.

Ukweli ni kwamba idadi kubwa ya Wamarekani bado walimpigia kura Donald Trump licha ya vitendo vyake miaka minne iliyopita, unaonyesha kile kinachokubalika nchini Marekani. Na hali hiyo inakatisha tamaa, bila kujali nani atakayeingia ikulu ya Marekani.

Mwandishi: Bleiker, Carla (DW Washington)
LINK: http://www.dw.com/a-55493212

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW