Maoni: Uchaguzi wa Uganda ni fursa iliyopotea
15 Januari 2021Ilikuwa dhahiri hata kabla ya kuanza kwa zoezi la uchaguzi kwmaba kinyang'anyiro kikubwa kingekuwa kati ya wagombea wawili - Yoweri Museveni dhidi ya Bobi Wine. Wagombea wengine tisa walikuwa wasindikizaji tu katika uchaguzi ulioshuhudia vurugu mbaya zaidi mpaka sasa tangu nchi hiyo ilipopata uhuru wake kutoka Uingereza mwaka 1960.
Licha ya kujitokeza kwa wingi kumchagua rais mpya, ni dhahiri tayari kwamba kufikikia mwisho wa kuhesabu kura Museveni atatangazwa mshindi.
Muda mfupi baada ya vituo vya kupigia kura kufungwa, mawakala wa Wine katika wilaya zisizopungua 22 walikuwa wakiandamwa na polisi na jeshi katika ukiukaji wa dhahiri wa taratibu za uchaguzi.
Aina hii ya vitisho ilionesha ni kiasi gani Museveni anaweza kutumia mamlaka yake, kinyume na katiba, kukandamiza upinzani hata katika siku ya uchaguzi.
Wakati matokeo yakitarajiwa mwishoni mwa wiki, Waganda wengi na hasa vijana wasio na ajira, wanatumai ushindi wa Bobi Wine utaleta mabadiliko wanayoyahitaji vibaya nchini humo.
Wanajifananisha na Wine katika njia nyingi kwa sababu anatokea ghetto, au makaazi ya mabanda kwama wao. Mbali na kufanana mambo mengi na Bobi Wine, vinaja wamechoshwa na mfumo ambao umeshindwa kuunda nafasi za ajira. Kukiwa na mfumo uliochoka wa afya, ukosefu mkubwa wa ajira na hali kubwa ya umaskini, wengi wanataka kubadilisha uongozi.
Hata wahitimu wa vyuo vikuu hivi sasa hawana ajira, Baadhi wamechagua kufanya kazi za ndani na udereva taxi katika mashariki ya kati kwa sababu hawaoni mustakabali wowote nyumbani.
soma zaidi: Bobi Wine adai kushinda wakati Museveni akiongoza
Rushwa iliyokithiri, ukosefu wa uwajibikaji katika ngazi za juu serikalini, na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu vimesababisha hali ya kukosa matumaini katika taifa ambalo waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Winston Churchill aliwahi kulielezea kama "Lulu ya Afrika."
Museveni asemekana kuidhibiti serikali
Museveni amegeuka kuwa serikali, na serikali imegeuka kuwa Museveni. Kama ilivyo kwa madikteta wengine, wakati wa uchaguzi, ana kauli ya mwisho katika masuala yote ya kitaifa.
Hakuna kinachoweza kufanyika bila idhini yake. Katika juhudi za kuwaweka kando waangalizi wa uchaguzi, Museveni aliamuru kusitisha kwa huduma zote za mitandao ya kijamii kama Twitter, Istagram na WhatsApp, baada ya mtandao wa Facebook kuzifunga akaunti zenye mafungamano na maafisa wa serikali na wanablogi waliokuwa wanasambaza taarifa za uongo.
Museveni amekuwa akitumia mbinu tofauti kusalia madarakani. Miongoni mwake ni ushoga, upendeleo wa kikabila, na kuunyima upinzani fursa yoyote ya kushirikiana na chama chake tawala. Anauchukulia upinzani kama maadui wa taifa na mawakala wa maslahi ya mataifa ya nje.
Amefanikiwa kuwanunua baadhi ya wanasiasa wa upinzani kw apesa kubwa na kuwapa nyadhifa za uwaziri katika serikali yake. Kwa mara kadhaa, Museveni amemtuhumu Bobi Wine kwa kutumikia maslahi ya kigeni na kuwatetea watu wanaoshirikia mapenzi ya jinsia moja katika taifa hilo la kihadhinia.
Licha ya visingizio hivyo visivyo na mashiko, Bobi Wine amefanikiwa kuvutia nadhari ya Waganda wengi na kote barani Afrika, kwa sababu ya utuhubutu wake wa kumtaka Museveni kupumzika. Museveni bado ana uungwaji mkono fulani katika maeneo ya vijijini ambayo yanamsifu kwa kuhakikisha amani na utulivu.
soma zaidi: Ni Museveni au Bobi Wine Uganda?
Mwisho, Museveni amehakikisha kuwa anaijaza tume ya uchaguzi wa watu watiifu kwake ambao watafanya vile atakavyo na kutangaza matokeo yanayomppendelea bila kujali chaguo la wananchi.
Itakuwa simulizi kubwa zaidi ya karne, iwapo tume ya uchaguzi ya Uganda itamtangaza Bobi Wine kuwa mshindi wa uchaguzi wa mwaka 2021.
Kwasasa, Bobi Wine anaweza kuanza kupanga kurudi kwake katika uchaguzi ujao wa mwaka 2025 wakati ambapo labda Museveni atakuwa amedhoofika sana kuwania tena jambo ninalolitilia shaka kwasababu azma yake ni kuondoka mamlakani wakati atakapokuwa ameiungaisha Afrika, hili likiwa jambo lisilowezekana.
Mwandishi: Isaac Mugabi/Tatu Karema