1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Itachukua muda mrefu kwa vidonda kupona

Zainab Aziz Mhariri: Josephat Charo
28 Mei 2021

Ujerumani sasa itaomba radhi rasmi kwa mauaji ya kimbari ya watu wa makabila ya Nama na Herero wa nchini Namibia.Kazi ya kufikia hatua hiyo ndiyo kwanza inaanza kutokana na masuala muhimu yanayopaswa kushughulikiwa.

Namibia, Windhuk I Denkmal zur Erinnerung an den Völkermord von Herero und Nama
Picha: Jürgen Bätz/dpa/picture alliance

Njia ya kulekea kwenye maridhiano baina ya Ujerumani na Namibia bado ni ya mashaka! Hata hivyo hatimaye Ujerumani imekubali kuyatambua rasmi mauaji ya watu wa makabila ya Nama na Herero. Hatimae rais wa Ujerumani atatoa tamko ambalo watu wa Namibia wamekuwa wanalisubiri kwa muda wa zaidi ya karne moja. Na hatimaye Ujerumani haitajaribu kuendelea kuficha au kupuuza uhalifu mkubwa uliotendwa na wajerumani nchini Namibia.

Soma Zaidi:Kwa kiwango gani Ujerumani inautambua uovu wa ukoloni wake?

Kwa mtazamo wa Ujerumani hiyo ni hatua muhimu. Msemaji wa rais wa Namibia ameeleza kwamba uamuzi wa Ujerumani wa kukiri kufanya mauaji hayo ya kimbari ni hatua inayolenga shabaha sahihi. Ni tamko la nadhari na staha ya kidiplomasia. Hata hivyo wawakilishi wa kabila la Herero bado wana dukuduku.Viongozi wa jadi wa makabila hayo  wameielezea hatua ya Ujerumani kuwa laghai, propaganda na ya kuwakejeli .Wanasiasa wa upinzani pia wameelezea mtazamo huo.

Rais wa Ujerumani Frank-Walter SteinmeierPicha: Bernd von Jutrczenka/dpa/picture alliance

Viongozi hao wa makabila ya Herero na Nama pamoja na wanasiasa wa upinzani walitaka kuhusishwa kwenye mazungumzo na serikali ya Ujerumani ana kwa ana. Hawana uhakika iwapo waherero na wanama ndio  watakaowekwa mbele ili kunufaika na mpango wa maendeleo ambao serikali ya Ujerumani imekubali kuutekeleza. Viongozi hao wana hasira kwa sababu serikali ya Ujerumani imekuwa inasisitiza mara kwa mara kwamba hakuna msingi wa kisheria juu ya fidia. Kulingana na mtazamo wao, serikali ya Ujerumani inaizingatia fidia hiyo kuwa kama zawadi!  Hata hivyo wapo baadhi ya viongozi wa waHerero na waNama wanaokubaliana na mkataba uliofikiwa lakini hakuna anayejua ni upande gani wenye idadi kubwa.

Angalia: 

Ujerumani yakubali kuyatambua mauaji ya kimbari ya Namibia

01:39

This browser does not support the video element.

Wajibu mkubwa sasa umo kwenye mikono ya serikali zote mbili. Kuomba radhi na maridhiano kutakuwa na  maana ikiwa idadi kubwa ya watu wa Namibia wataridhia. Msingi wa hilo ni kuaminiana.Tunatumai kwamba rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier atatamka maneno yanayostahili. Fursa ipo. Rais Steinmeier ni mtu anayetambua nguvu ya maneno na hivyo kuyatumia mahala panapostahili na kutoa ujumbe sahihi.

Ishara ni muhimu. Kuomba radhi kwenye bunge la Namibia kutakuwa fursa muhimu lakini pia itakuwa muhimu ikiwa ataomba msamaha pale ambapo wajerumani walitenda uhalifu, kwenye maeneo ya waHerero na waNama, kwenye kumbumbuku za wahanga na mbele ya vizazi vyao.Ni baada ya hatua hizo kuchukuliwa ndipo kazi itaanza kwa uhakika.Waliofanyiwa ukatili ndiyo wanaopaswa kukumbukwa kwenye mitaa na minara ya kumbukumbu nchini Ujerumani bila ya kinyongo, na siyo wakoloni.

Rais wa Namibia Hage GeingobPicha: AFP/R. Bosch

Mauaji ya kimbari yaliyofanywa na wajerumani nchini Nambia yanapaswa kuwa sehemu ya ufahamu wa watoto shuleni nchini Ujerumani. Watalii wa Ujerumani watapaswa pia kuangazaia historia ya ukatili wa wajerumani na siyo tu kuyatembelea majengo ya enzi ya ukoloni.

Maridhinao yatakuwa na maana ikiwa rais wa Ujerumani, serikalina idadi kubwa ya wajerumani wataitilia maanani historia yao nchini Namibia. Maridhiano pia yatakuwa na maana ikiwa watu wa Namibia, na hasa waHerero na waNama watakuwa na imani kwamba Ujerumani ina dhamira ya kweli.

Njia ya kufika kwenye lengo hilo bado ni ndefu.!  

Chanzo:/ LINK: Meinung: Versöhnung nach dem Völkermord an Herero und Nama in Namibia

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW