1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulio ya kigaidi Tunisia

Admin.WagnerD19 Machi 2015

Wahariri wa magazeti leo wanazungumzia juu ya mashambulio yaliyofanywa na magaidi nchini Tunisia na juu ya maandamano ya kuzipinga sera za Benki Kuu ya Ulaya ECB

Mashambulio ya kigaidi kwenye nyumba ya makumbusho mjini Tunis
Mashambulio ya kigaidi kwenye nyumba ya makumbusho mjini TunisPicha: AFP/Getty Images/F. Belaid

Gazeti la "Eisenacher Presse" linasema juu ya mashambulio yaliyofanywa na magaidi kwenye nyumba ya makumbusho katika mji mkuu wa Tunisia, Tunis , kwamba magaidi wanawashambulia siyo tu waandishi wa habari bali pia watu wasio na hatia kama watalii.

Mhariri huyo anasema Tunisia ni nchi iliyoanza kutoa mfano bora kwa kuanza kuelekea kwenye uhuru na usalama ,wakati katika nchi kama Syria, Libya na Yemen vurumai zimeshtadi.

Mhariri wa gazeti la "Rhein-Necker" anaeleza kwamba mashambulio yaliyofanywa na magaidi nchini Tunisia yanaweza kuwa ishara ya mwisho wa vuguvugu la mapinduzi katika nchi za kiarabu.

Mhariri huyo anasema ikiwa Tunisia nayo itaeguka kuwa nchi isiyokuwa na usalama kama vile Libya na Algeria basi hali hiyo inanaweza kuwa ishara ya mwisho wa harakati za kuleta mapinduzi katika nchi za kiarabu. Lakini mahariri amesema inapasa kukiri kwa mtazamo wa leo kwamba tokea mwanzo kabisa harakati hizo zilikuwa ndoto tupu.

Mhariri anatilia maanani kwamba harakati hizo hazikuleta ukombozi katika Afrika Kaskazini wala katika Mashariki ya Kati. Baada ya kuondoka madikteta, wamekuja magaidi.


Na mhariri wa gazeti la "Badisches Tagblatt" anasema shambulio la kigaidi nchini Tunisia ni pigo kubwa kwa demokrasia nchini humo. Sasa pana hatari kubwa ya kutifuka wimbi la mauaji nchini Tunisia.

Sera za Benki Kuu ya Ulaya zapingwa

Wapinzani wa ubepari walifanya maandamano ya kuzipinga sera za Benki Kuu ya Ulaya kwenye makao makuu ya Benki hiyo mjini Frankfurt. Ghasia kubwa zilitukia.

Gazeti la "Badische Neueste Nachrichten" linasema hakuna kinachoweza kuzihalalisha ghasia zlizotukia kwa sababu waandamanaji waliivuka mipaka.Ghasia hizo zimezigubika hoja za watu hao za kuzipinga sera za Benki Kuu ya Ulaya.

Mhariri wa gazeti la "Thüringische Landeszeitung" anasema , licha ya sera ya Benki Kuu ya Ulaya ya kuzaja fedha kwenye mabenki ,kuwa ya utatanishi, sera hiyo imezisaidia nchi zenye matatizo ya fedha. Mhariri wa gazeti hilo anaeleza kwamba mpango wa Benki Kuu ya Ulaya úmezisaidia nchi zenye matatizo makubwa ya kiuchumi. Bila ya msaada mkubwa wa fedha kutoka Benki Kuu ya Ulaya nchi kama Ugiriki ingelifilisika siku nyingi, na umasikini ungelikuwa mkubwa zaidi nchini humo.

Mwandishi:Mtullya Abdu. /Deutsche Zeitungen.

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW