1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni ya wahariri juu ya mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje juu ya Ukraine

Abdu Said Mtullya3 Julai 2014

Mawaziri wa mambo ya nje wa Urusi,Ufaransa, Ukraine na Ujerumani wamekutana Berlin kuujadili mgogoro wa Ukraine.Wahariri wa magazeti wanatoa maoni yao.

Mawaziri wa mambo ya nje kwenye mkutano wao mjini Berlin
Mawaziri wa mambo ya nje kwenye mkutano wao mjini BerlinPicha: picture-alliance/dpa

Gazeti la"Volksstimme" linasema mawaziri wa mambo ya nje walikubaliana mjini Berlin juu ya ulazima wa kusimamisha mapigano mashariki mwa Ukraine.Juu ya mkutano huo mhariri wa gazeti la "Volksstimme" anaipongeza Ujerumani kwa juhudi zake zenye lengo la kuutatua mgogoro wa nchini Ukraine. Mhariri huyo anatilia maanani kwamba juhudi za Ujerumani zimewaleta pamoja mawaziri wa mambo ya nje wa Urusi na Ukraine.


Mhariri huyo anasema ni kweli kwamba ,Urusi na Ukraine zimeelewana juu ya haja ya kusimamisha mapigano, lakini anasema muhimu zaidi ni kwa watu wa Ukraine wenyewe kuwa na dhamira ya kuutatua mgogoro wa nchi yao.

Mvutano mkubwa katika Mashariki ya Kati

Gazeti la "Hessische Niedersächsische Allgemeine" linauzungumzia mvutano mkubwa uliopo sasa katika Mashariki ya Kati kufuatia vifo vya vijana wa Kiyahudi na Kipalestina.Mhariri wa gazeti hilo anasema kwamba Waisraeli na Wapalestina kwa mara nyingine wamesimama mkabala.

Gazeti linatahadharisha ,chonde chonde, watu wenye siasa kali, waliopo katika kila upande wasiruhusiwe kuanzisha vita nyingine. Na kwa hivyo ni jambo la kutiliwa maanani kwamba mpaka sasa majeshi ya Israel bado hayajaingia katika Ukanda wa Gaza, licha ya ghadhabu ya Waisraeli iliyosababishwa na kuuliwa vijana watatu wa kiyahudi.


Mhariri wa gazeti la "Märkische Oderzeitung" leo analizingatia suala la wakimbizi waliopo nchini Ujerumani. Hivi karibuni palitokea mvutano baina ya wakimbizi na idara za serikali, katika kitongoji kimoja cha mji wa Berlin kinachoitwa Kreuzberg. Kutokana na makaazi mabaya waliopewa, wakimbizi hao waliamua kuivamia shule na kuishikilia.Mhariri wa "Märkische Oderzeitung" anatoa maoni yake.

ABDU:

Wakimbizi ni watu wanaozikimbia hali za hatari ili kuyaokoa maisha yao na kuanza maisha mapya kwingineko. Ukweli huo pia unawahusu wakimbizi wanaokuja Ujerumani.Lakini wajerumani mara nyingine wanasema hilo haliwezekani.Ni kweli kwamba wapo wakimbizi bandia.Na wapo wale wanaovunja sheria wanapokuwamo nchini.

Lakini tatizo kubwa ni kwamba serikali haiwaelezi wakimbizi juu ya wajibu wao na kwamba wanaweza kufukuzwa nchini.

MODE:
Mhariri wa gazeti la "Märkische Oderzeitung" anasema matukio ya mjini Berlin, ambapo wakimbizi waliivamia shule moja na kuishikilia, yameonyesha nini kinaweza kutokea ikiwa wakimbizi hawaujui wajibu wao.

Concl....huo ulikuwa muhtasari wa maoni ya wahariri.

Mwandishi:Mtullya Abdu./Deutsche Zeitungen.

Mhariri: Josephat Charo

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW