Maoni ya wahariri juu ya unyama wa Boko Haram
16 Aprili 2014Mhariri wa gazeti la "Landeszeitung Lüneburg" anasema miaka ishirini baada ya kutokea mauji ya kimbari nchini Rwanda, jumuiya ya kimataifa inayashuhudia maujai mengine barani Afrika.
Mauaji hayo hayatokei katika nchi ndogo iliyojibanza milimani. Mauaji hayo yanatokea, Nigeria nchi kubwa , siyo tu kutokana na idadi kubwa kabisa ya watu barani Afrika bali pia ,siku chache tu zilizopita Nigeria ilitangazwa kuwa nchi yenye nguvu kubwa za kiuchumi kuliko nyingine yoyote barani Afrika.
Mhariri wa gazeti la "Landeszeitung Lüneburg" anasema Kundi la Waislamu wanaoifuata itikadi kali, Boko Haram, limefungulia wimbi la umwagijaki damu kaskazini mwa Nigeria.
Utawala wa Kiislamu
Watu hao wanataka kuanzisha utawala wa kiislamu.Mhariri anasema serikali ya Nigeria haina dhamira wala nguvu za kuyatatau matatizo ya nchi.Anasema Nigeria inaonyesha dalili zote za nchi inayoyumbayumba.
Gazeti la "Mittelbayerische" linauzungumzia uchaguzi ujao, wa Bunge la Ulaya,kwa kuwakumbusha wananchi umuhimu wa kupiga kura. Mhariri wa gazeti hilo anasema Umoja wa Ulaya ni jumuiya, siyo tu ya kiuchumi yenye nguvu za kushindana na mataifa mengine duniani bali pia ni jumuiya yenye tunu zinazowahamasisha hata watu nchini Ukraine, kuzipigania haki zao.
Na kwa hivyo yeyote anaeukosoa Umoja wa Ulaya hana budi akumbuke kupiga kura tarehe 25 mwezi ujao.Kutofanya hivyo na badala yake kulalamika tu, siyo jambo la kiungwana.
Hukumu ya Berlusconi ni kashfa
Gazeti la "Braunschweiger" linazungumzia juu ya adhabu aliyopewa aliekuwa Waziri Mkuu wa Italia Silvio Berlusconi. Mwanasiasa huyo amepewa adhabu ya kufanya kazi za kijamii kwenye nyumba za matunzo ya wazee kwa muda wa mwaka mmoja .Lakini mhariri wa gazeti la "Brauschweiger" anasema kutokana na uzito wa uhalifu alioutenda, adhabu hiyo siyo ya haki. Ni aibu!
Mwandishi:Mtullya Abdu/Deutsche Zeitungen.
Mhariri: Mohammed Abdul-rahman