1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kashfa ya kukwepa kulipa kodi

Admin.WagnerD5 Aprili 2016

Wahariri wanatoa maoni juu ya kashfa iliyofichuliwa katika kinachoitwa nyaraka za Panama zinazotaja kampuni,majina ya watu mashuhuri na wanasiasa wanaoficha mali zao nje ya nchi zao ili kukwepa kulipa kodi.

Picha ya ishara ya kashfa ya kukwepa kulipa kodi
Picha ya ishara ya kashfa ya kukwepa kulipa kodiPicha: picture-alliance/maxppp/J. Pelaez

Mhariri wa gazeti la "Braunschweiger" anasema ni kiwango cha kashfa iliyofichuliwa kinachoudhi sana. Ansema ni uzembe wa idara husika duniani kote unaowafanya watu waingiwe utasi.! Mawaziri,wafalme, marais,mamilionea na wanamichezo maarufu kutoka duniani kote wametajwa kuhusiana na kashfa ya nyaraka za Panama.

Mhariri wa gazeti la "Braunschwiger " anasema watu hao wanalenga shabaha moja tu :kuficha utajiri wao. Idara za kodi zimeshtushwa duniani kote na kiwango cha kashfa. Gazeti hilo linasema sasa wahusika hawawezi tena kutazama pembeni. Lazima hatua zichukuliwe.

Gazeti la "Braunschweiger" linasema mabenki 15 ya Ujerumani yamehusishwa na kashfa ya Panama. Kampuni bandia au mashirika ya hisani yanayoongozwa na watu wasiokuwa na majina lazima yapigwe marufuku.

Wahalifu wako hatua nyingi mbele ya wachunguzi

Gazeti la "Badische" linatilia maanani kwamba watu wanaofanya biashara za kizani siku zote wako hatua kadhaa mbele ya wachunguzi. Hata hivyo mhariri wa gazeti hilo anasema haitakuwa sawa kushika tama.

Rais wa Ukraine Petro Poroshenko pia anatuhumiwa kuficha mali nje ya nchiPicha: DW/Y. Bojko

Mhariri huyo anaeleza kuwa kila inapopatikana njia ya kuwagundua watu hao,nao pia wanavipata vipenyo vipya. Anasema hili ni jambo la kukasirisha lakini watu wasikate tamaa. Mhariri wa gazeti la "Badische anawapongeza watu wanaozifichua siri za biashara za kizani.

Gazeti la "Der neue Tag" linasema kilichofichuliwa katika nyaraka za Panama siyo jambo la ajabu lakini linaudhi. Mhariri wa gazeti hilo anaeleza kwamba uroho wa mali na mamlaka hauna mwisho. Wafanyabiashara na wanamichezo wanachezea mabilioni ya fedha .

Gazeti hilo linasema wanasiasa wa nchi za magharibi pia wametajwa katika nyaraka za Panama. Sasa umefika wakati wa kuzungumzia kwa moyo mmoja juu ya suala la uadilifu miongoni mwa matajiri wakubwa katika jamii.Gazeti la "Der neue Tag " linaendelea kusema ni kweli kwamba suala hilo limekuwa linajadiliwa, lakini siyo kwa uthabiti wote.

Mhariri wa gazeti la "Badische Neueste Nachrichten" anatanabahisha kwamba, iwe ni Ulaya, Afrika ,Marekani na kwingineko, matajiri siku zote wanapata mahala pa kuyaficha magunia yao ya fedha ili yasilowane.

Mwandishi: Mtullya Abdu.

Mhariri: Daniel Gakuba