Maoni ya wananchi kuhusu hotuba ya Rais Karume wa Zanzibar
23 Novemba 2009Matangazo
Rais Karume alitangaza mwanzo mpya wa kuondoa uhasama kati ya chama cha CUF upinzani na chama tawala cha CCM. Vyama hivyo viwili kwa miaka mingi vimekuwa na uhasama ,huku tofauti zao za kisiasa zikiwaathiri kwa kiasi kikubwa wananchi wa visiwa hivyo.
Katika kukusanya maoni ya wananchi hao kwanza ni msikilizaji Fred Khamisi Hamadi kutoka eneo la Chemi Chemi visiwani humo.
Mkusanyaji : Jane Nyingi
Mpitiaji:Aboubakary Liongo