Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta amesaini mkataba wa miaka minne na nusu wa kuichezea timu ya Aston Villa ya Uingereza. Samatta mwenye umri wa miaka 27, anakuwa Mtanzania wa kwanza kuchezea Ligi Kuu ya England akitokea kwenye timu ya Genk ya Ubelgiji.