1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapambano baina ya vyama vya Fatah na Hamas yazidi huko Palastina.

17 Desemba 2006

Gaza:

Mwanajeshi katika kikosi kinachomlinda Rais Mahmud Abbas wa Palastina ameuliwa na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika mapambano na wafuasi wa chama tawala cha Hamas. Michafuko hiyo mipya katika Ukanda wa Gaza ilitokea masaa baada ya rais wa Wapaalstina, Mahmud Abbas, ambaye anaungwa mkono na chama cha fatah, kutangaza kwamba anataka kuitisha uchaguzi wa mapema wa urais na bunge ili kuutanzua mzozo ulioko baina ya chake cha Fatah na Hamas. Chama cha Hamas kimesema hatua hiyo ya rais ni kama kufanya mapinduzi. Mahmud Abbas hajataja tarehe ya kufanyika uchaguzi huo, na amesema bado yuko tayari kufanya mazungumzo na Chama cha Hamas juu ya kuundwa serekali ya Umoja wa Taifa.

Waziri mkuu wa Uengereza, Tony Blair, amezihimiza serekali kote duniani zimuunge mkono rais wa Wapalastina, Mahmud Abbas. Kiongozi huyo wa Uengereza hivi sasa yuko Misri akifanya ziara katika Mashariki ya Kati ambapo amepangiwa kufanya mazungumzo na viongozi wa Kipalastina na Wa-Israeli mnamo siku zijazo. Pia Marekani na Umoja wa Ulaya zimelipokea kwa uzuri tangazo la Rais Mahmud Abbas la kutaka kuitisha uchaguzi wa mapema. Msemaji wa Ikulu ya Marekani alisema serekali ya nchi yake inataraji michafuko katika maeneo ya Wapalastina itakoma. Mwanadiplomasia mkuu wa Umoja wa Ulaya, Javier Solana, amemhakikishia Mahmud Abbas kwamba Umoja wa Ulaya unamuunga mkono.