MAPAMBANO KUSINI MWA NIGERIA:
6 Desemba 2003Matangazo
LAGOS: Si chini ya watu wanne wameuawa,baada ya vikosi vya Nigeria kukivamia kijiji kimoja katika eneo la kusini lenye utajiri wa mafuta.Kwa mujibu wa duru za kabila la Ijaw mapambano mapya yalizuka kati ya makundi yanayohasimiana.Na mwanaharakati anaepigania haki za binadamu katika eneo hilo Joel Bisina amesema vijana wa kabila la Itsekiri walifuatana katika motaboti 36 na waliishambulia jamii ya kabila la Ijaw.Baadae helikopta ya kijeshi ilikwenda katika kijiji kingine na kufyetua risasi.Watu wanne waliuliwa katika shambulio hilo.Lakini mwanachama mmoja wa kikundi cha wanamgambo wa kabila la Ijaw,amesema idadi ya watu waliofariki katika mapambano hayo na jeshi si chini ya 50.Maafisa wa kijeshi hawakupatikana kutoa maelezo.Eneo la kusini la Niger Delta likiwa na utajiri mkubwa wa mafuta,limeshuhudia machafuko tangu mwezi Machi,pale Wa-ijaw walipoanzisha uasi dhidi ya kabila la Wa-itsekiri,jeshi na makampuni ya kimataifa ya mafuta.